Wema Sepetu: Nina miezi 5 tangu niache kutumia pombe

Hata hivyo, Sepetu hakutaja sababu zilizomfanya kuacha pombe.

Muhtasari

• Mwigizaji huyo aliyasema haya baada ya kukutana na mtangazaji mwatukaji wa Clouds, Mwijaku Burton.

Wema Sepetu asema hajawahi tumia pombe kwa miezi 5.
Wema Sepetu asema hajawahi tumia pombe kwa miezi 5.
Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe wa filamu za Bongo Wema Abraham Sepetu amefunguka kuwa ana takribani nusu mwaka tangu aache kutumia vileo vya aina yoyote.

Mwigizaji huyo aliyasema haya baada ya kukutana na mtangazaji mwatukaji wa Clouds, Mwijaku Burton ambaye alimfurahia na mpaka kumbeba juu kwa juu akimhongera kwa kupendeza.

Mwijaku kwa kuropojkwa kwake alisema kwa kuradidi kwamab Wema Sepetu ameacha pombe na Sepetu mwenyewe akadakia kuwa ana miezi mitano tangu afunge ukurasa wa pombe katika maisha yake.

“Niwaambie tu kitu kimoja ni kwamba Wema kaacha pombe,” Mwijaku alisema huku akimpakata Wema mikononi mwake kama mtoto mdogo na kufanya mzunguko wa mvirinyo naye huku mbwa wake Manunu akiwabwekea na kuwarukia akidhani ni mchezo wanacheza.

“Nina miezi mitano tangu niache kutumia pombe, si unaona vile niko vizuri nimependeza,” Wema alimwambia Mwijaku.

Lakini si Wema Pekee ambaye amejitokeza wazi na kukiri kwamab ameach kutumia pombe.

Nchini Kenya, maceleb kadhaa wamewahi jitokeza na kukiri kuacha pombe akiwemo watangazaji Alex Mwakideu, Wilbroda na wasanii kama vile DNA, Frasha, Kabi wa Jesus, Natalia Tewa miongoni mwa wengine.

Mwakideu na mwenzake Jalang’o walisema kuwa walikuwa tayari kuacha kutumia vileo na kutumia rasilimali hizo katika kuendeleza miradi yao ya ujenzi katika kaunti ya Kajiado, eneo la Kitengela.

Kabi wa Jesus naye alisema kuwa alilazimika kuacha ulevi mwaka 2013 na kumkimbilia Mungu baada ya kugundua kuwa ulevi ulikuwa unamgharimu sit u kimfuko bali pia kiafya.