Jaguar aibua maswali akionekana na mrembo, helikopta na magari ya kifahari

Jaguar walikuwa wameshikana na mrembo huyo kimahaba huku wakiongoozana kuelekea kwa meza iliyofunikwa na vinywaji ghali.

Muhtasari

• Nyuma yao, kulikuwa na magari mawili ya kifahari na mezani chupa na bilauri zilizomiminiwa vinywaji hivyo ghali.

Jaguar akipunja maisha na mrembo asiyejulikana.
Jaguar akipunja maisha na mrembo asiyejulikana.
Image: Facebook

Msanii mkongwe kutoka nchini Kenya Charles Njagua Kanyi almaarufu Jaguar amezua maswali mengi kuliko majibu mitandaoni baada ya kuonekana akila bata katika sehemu ya mikutano ya faragha na mrembo asiyetambulika lakini pia na vitu vya thamani kama magari vinywaji bila kusahau ndege aina ya helikopta.

Katika picha hizo tatu ambapo Jaguar alizichapisha kwenye kurasa zake mitandaoni, ya kwanza ilimuonesha akitembea na mrembo huyo kutoka kwa helikopta, huku wameshikana mikono wakiongozana kwenda katika meza iliyokuwa imeandaliwa na vyakula vya aina mbalimbali.

Image: jaguar,

Picha ya pili na ya tatu ziliwaonyesha wawili hao wameketi mezani mkabala kutoka kwa kila mmoja wakifanya mazungumza huku meza ikiwa imefunikwa na vinywaji na nyuma yao kulikuwa na magari mawili ya kifahari.

Jaguar hakutoa ufafanuzi wowote kuhusu matukio katika picha hizo bali aliandika kapsheni kama ya kutoa himizo hivi akiwashauri wafuasi na mashabiki wake kutokengeushwa na kitu chochote na badala yake kubaki katika uhalisia wao tu.

“Hakuna mtu anayeweza kuwa wewe bora kuliko wewe mwenyewe,” Jaguar aliandika.

Image: jaguar

Hata hivyo, picha hizo ziliibua maswali mengi, watu wakishindwa kumtambua kwa mara moja mrembo huyo alikuwa nani, kwani inafahamika Jaguar ni baba mwenye familia ya watoto watatu na huwa hapendi kupakia mambo ya kifamilia mitandaoni.

Wengine pia walihisi Jaguar ni kama amerejea kwenye muziki na ni sehemu ya video ya wimbo wake ambapo alikuwa anamshirikisha mrembo huyo kama vixen.

Na wengine waliibuka na dhana kwamba helikopta ile ni ya mwandani wake rais William Ruto ,kwani ilishabihiana kwa sehemu kubwa na yake.