Pierra Makena atoa onyo kali kwa watu wanaoiga wazo lake la Park & Chill

Makena alisema watu wanaoiga na kuchapisha misimbo na nukuu zake wamekosa ubunifu huku akiwaonya vikali.

Muhtasari

• "Mbona watu wasije na mawazo yao ya kibunifu badala ya kuiga? " Pierra mwenye hasira aliandika kwenye Instastory yake.

Image: instagram

Mcheza santuri maarufu wa kike, Pierra Makena ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa hasira ya muda mrefu kueleza kusikitishwa kwake na ukosefu wa ubunifu katika tasnia hiyo na watu kuiba dhana yake na kuipitisha kama yao.

Makena mwenye umri wa miaka 42 ambaye pia ni mwigizaji na mfawidhi alishiriki kwamba kuiga na kuchapisha kulionyesha vibaya tasnia ya burudani nchini Kenya na kumwacha na tope usoni.

"Enyewe tasnia yetu imechafuliwa!' Makena alisema.

Aliendelea kuongeza kukerwa kwake na kile anachotaja kama ukosefu wa uhalisia wa watu.

"Mbona watu wasije na mawazo yao ya kibunifu badala ya kuiga? Sasa leo nimeona chill na vibe, jana niliona Park na chew  kisha juzi Park na Vibe... yaani inamaanisha kwamba hivyo ndivyo tulivyo na mawazo finyu?" Pierra mwenye hasira aliandika kwenye Instastory yake.

Mama huyo wa binti mmoja ni maarufu kwa kuongoza tafrija na matamasha kama DJ kwenye Park na Chill ambapo washereheshaji hujitokeza na magari yao na kujivinjari huku wakifurahia ustadi wake katika kupakua burudani

Mama Pokot akionyesha masikitiko yake alitaja kuwa watu hawa walio na nia ya kuchukua wazo lake la ubunifu kama lao wamefikia hatua ya kumfanya atiwe mbaroni kwa sababu walidhani ni mnyonge.

"Halafu unaiga kila kitu ingine.....na kwa sababu unafikiri una mamlaka zaidi unawatafuta wanawake waliopoteza matumaini maishani kwa sababu unafikiri hawawezi kujipigania. Na haswa wacheza santuri wa kiume ambao kila mara wanafanya makusudi kuangusha ushindi wangu....subirini," Makena alicharuka.

Image: Pierra Makena