Kabi WaJesus azungumza baada ya kurushiwa cheche za matusi kuhusu video aliyotengeneza na mama mkwe

Kabi alizungumzia hali ya kutoridhika iliyotokana na video ambazo amekuwa akitengeneza na mama mkwe wake alizozipakia kwenye Tiktok.

Muhtasari

•  Kabi Wa Jesus alitetea nyakati zao za kufurahisha zilizonaswa kwenye video hizo, jambo ambalo halikuwafurahisha baadhi ya mashabiki wake wa Tiktok.


Kabi wajesus
Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Kabi WaJesus ambaye ni mwanablogu, alizungumzia hali ya kutoridhika iliyotokana na video ambazo amekuwa akitengeneza na mama mkwe wake alizozipakia kwenye Tiktok.

Huku akionyesha upendo na mapenzi yake kwa Bi. Ng'ang'a, Kabi Wa Jesus alitetea nyakati zao za kufurahisha zilizonaswa kwenye video hizo, jambo ambalo halikuwafurahisha baadhi ya mashabiki wake wa Tiktok.

Kwenye video hiyo alieleza kuwa amegundua kuwa baadhi ya mashabiki wake  hawajafurahishwa na hiyo video anajua wameumia kwa sababu anaelewa wamepitia mengi katika maisha yao na fikra zao ni finyu.

"Nilihisi kutaka kuomba msamaha kwa sababu niligundua kuwa timu yangu ya mtandao iliwajibu kila mtu ambaye alileta maoni hasi yoyote ila siombi msamaha kwa masaibu yasiyokuwa yangu.

Bi. Nganga nakuja ili tufanye tiktok nyingine na tutavuma," Kabi aliongezea.

Akisisitiza kwa ukaidi kwamba hakuna maoni ya yeyote yanayoweza kuathiri uhusiano wake na mama mkwe wake, Kabi Wa Jesus alichukua msimamo wa kuchekesha lakini thabiti kwa kupendekeza kwamba wale wasiokubaliana na video zake watafute mwongozo kutoka kwa mababu zao.

"Kwa hivyo,timu yangu ya mitandao ya kijamii wape dawa unayostahili kuwapa," alisisitiza mume wake Milly.

Baadhi ya maoni yaliyotolewa na mashabiki wake Kabi yalikuwa kama yafuatayo:

"Weeee!!! Hapana!!! Kuna boundaries na mother in law...hii hapana," Amito aliandika.

"Boundaries muhimu hata kama wazazi wengine wametutufeli kwa sababu ya kukuwa celeb wamesahau utamaduni," aliandika Nancy Ireri.