Mwanamume wangu akiacha kunitumia pesa nitamuacha bila kufikiria mara mbili - Jackie Matubia

Katika video hiyo ya kuiga kwenye TikTok, Matubia alisema suala la kumtema mwanamume asiyetumia pesa zake kwake ni rahisi kama ABC.

Muhtasari

• Matubia na mpenzi wake Blessing Lung'aho wamekuwa wakisemekana kutokuwa na maelewano katika siku za hivi karibuni.

• Wenzi hao walianza kuchumbiana mnamo Februari 2021 na hivi majuzi walisherehekea kumbukumbu yao ya pili.

Wapenzi waigizaji Lungaho na Matubia
Wapenzi waigizaji Lungaho na Matubia
Image: YouTube screengrab

Mwigizaji Jackie Matubia amedai kuwa yeye hawezi kuendelea katka uhusiano na mwanamume ambaye ameacha kumtumia hela za matunzo na matumizi mengine.

Mwigizaji huyo katika klipu aliyoipakia kwenye Tiktok yake akiiga sauti ya mwanamke mwingine, alisema kuwa hawezi hata fikiria mara mbili kuhusu hatima ya uhusiano wake na mwanamume wake, ikiwa mwanamume huyo ataweka kikomo katika kumpa hela.

“Nitamuacha mapema mapema, nitamblock na kusema kweli siwezi kuwa na biashara yoyote na mtu ambaye hataki kutumia pesa zake kwangu. Ni rahisi kama ABC…” Jackie Matubia aliiga sauti hiyo.

Kwa muda wa wiki kadhaa sasa, Matubia na mpenzi wake Blessing Lung’aho wamekuwa wakisemekana kutokuwa katika hali sawa, mashabiki wao wakihisi kuwa huenda wawili hao wameachana kinyemela.

Hata hivyo, Matubia katika mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha redio humu nchini alifutilia mbali uvumi huo akisema kuwa wako sawa na Lung’aho lakini pia alionekana kutotaka kuzungumzia mengi kwa kina kuhusu hali ya uhusiano wao.

Mashabiki walianza kuhisi mambo si shwari katika uhusiano wao baada ya Matubia kupakia klipu kwenye Tiktok yake akiiga sauti ya mtu ambaye alikuwa ameulizwa uhakika kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na kusema kuwa hakuwa na uhakika wowote kuhusu mapenzi.

Katika video hii, alizungumza kuhusu kosa alilofanya na jinsi ambavyo hangeweza kupona kutokana nalo.

“Nilikuwa nafikirianga ni mimi pekee yangu huwa naitwa babyghurl na nikafanya makosa nikashika simu yake,” Matubia alidokeza kiini cha uvumi wa kuachana kwao.

Wenzi hao walianza kuchumbiana mnamo Februari 2021 na hivi majuzi walisherehekea kumbukumbu yao ya pili.