Eric Omondi na Amber Ray kuachia kibao cha pamoja

"Wimbo wenyewe unaitwa "you are all P*ssies," Eric alisema kwa mbwembwe.

Muhtasari

• Katika hiyo video Omondi alidai kuwa sababu yake ya kutoa huo wimbo ni kuwaonyesha wasanii wa Kenya jinsi video inavyopaswa kukuwa.

• "Wimbo wenyewe unaitwa "you are all P*ssies," Eric alisema kwa mbwembwe.

Eric Omondi na Amber Ray kuachia kibao cha pamoja.
Eric Omondi na Amber Ray kuachia kibao cha pamoja.
Image: Instagram

Siku ya Jumanne, mchekeshaji Eric Omondi aliweka wazi katika kufanya kolabo na mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray.

Hili linajiri baada ya Eric kupakia video katika ukurasa wake wa Instagram akielezea kuwa kibao ambacho alimshirikisha Amber  Ray. 

Kibao hicho kinatarajiwa kuachiliwa mnamo siku ya Ijumaa saa nne asubuhi.

Katika hiyo video Omondi alidai kuwa sababu yake ya kutoa huo wimbo ni kuwaonyesha wasanii wa Kenya jinsi video inavyopaswa kufanywa. 

Aliongezea na kusema kuwa alitoa shilingi milioni 3.8 kufanya hiyo video na sauti hiyo ilirekodiwa nchini Afrika kusini na kuboreshwa nchini Marekani.

Omondi alidai kuwa amefanya video ambayo hata Chris Brown hawezi fanya.

Omondi ambaye hivi karibuni amedokeza kuacha ucheshi na kuwa mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu alidai kuwa amechagua na kumchukua msichana mwenye talanta bora na mrembo zaidi ambaye anatoa nyoka pangoni.

Naye mwanasosholaiti Amber Ray aliongezea kwa mbwembwe na kusema, " hapo sasa lazima tuwaonyeshe hii kazi mnafanya hapa haiwezi."

Katika video hiyo aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Eric alisema kuwa kuwa hana muda ya kuwabembeleza wanaume wavivu na kudai kuwa alipigania wasanii kule kwa bunge ila hawamsaidii na wanamuaibisha.

"Siku ya Ijumaa mnamo saa nne asubuhi mtaona video halisi ni nini na hii itaingia hadi Nigeria na wimbo wenyewe unaitwa "you are all P*ssies," Eric alisema kwa mbwembwe.