Uliokoa maisha yangu na niko hapa na wewe milele - ujumbe mtamu wa Rotimi kwa Vanessa

"Nakupenda sana. Safari hii pamoja nawe imekuwa Baraka kutoka kwa Mungu. Ninashukuru sana kuwa na wewe," aliandika kwa sehemu.

Muhtasari

Katika ujumbe huo mzito, Rotimi alionyesha kuvutiwa kwake na Vanessa, akimtaja kuwa shujaa wa maombi.

Rotimi ammwagia makopakopa mpenzi wake Vanessa Mdee siu yake ya kuzaliwa.
Rotimi ammwagia makopakopa mpenzi wake Vanessa Mdee siu yake ya kuzaliwa.
Image: Instagram

Siku moja iliyopita, aliyekuwa malkia wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameolewa marekani alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Mpenzi wake Rotimi ambaye pia ni msanii aliwakosha wengi mioyo kwa kumuandikia mama watoto wake wawili ujumbe wa kufurahisha kwenye Instagram, akimtaja kuwa mwanamke shupavu ambaye ni jasiri na shujaa katika maombi.

Katika ujumbe huo mzito, Rotimi alionyesha kuvutiwa kwake na Vanessa, akimtaja kuwa sio tu rafiki yake mkubwa bali pia chanzo cha nguvu na bidii zake katika mishe mishe zake kutoka muziki hadi kwenye uigizaji.

Aliendelea kuangazia uzuri wake wa ndani na nje, akisisitiza athari kubwa aliyonayo katika maisha yake. Alisifu uzazi wa kipekee wa Vanessa na usaidizi usioyumbayumba kama mshirika, akimhakikishia upendo wake usio na mwisho.

"Kwa hadithi hai, rafiki yangu mkubwa, shujaa wa maombi, mwanamke mzuri zaidi, mama wa ajabu, na mwenzangu. Nakupenda sana. Safari hii pamoja nawe imekuwa Baraka kutoka kwa Mungu. Ninashukuru sana kuwa na wewe," aliandika kwa sehemu.

Wanandoa wa nguvu, Rotimi na Vanessa, wameonyesha mapenzi yao ya kina bila kusita.

Kila hatua muhimu inaonyeshwa na maonyesho ya kupita kiasi ya upendo, na kuwaacha mashabiki na shangao la ishara zao za kutoka moyoni.

Katika chapisho hilo, Rotimi alikiri kwamba Vanessa alibadilisha maisha yake tangu siku ambayo wawili hao walikutana.

"Uliokoa maisha yangu na niko hapa na wewe milele. Happy birthday mama Imani,” aliongeza.

Kujitolea kwa Rotimi kwa Vanessa hakuna kikomo, kwani yeye humwagilia zawadi za gharama kila mara na hadharani ili tu kuthamini uwepo wake katika maisha yake.

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa miaka michache lakini tayari wamebarikiwa na watoto wawili ambao hawachoki kuonyesha Baraka hizo zao mitandaoni kwa upendo kila mara.