Jalang'o umesahau mahali ulitoka sasa hivi umewaruka 'content creators' - Gaucho

“Wewe ukijua kwanza sasa hivi unakula pesa bure, surely Jalang’o, unasahau mahali umetoka, mahali pa kufeki maisha sasa hivi unaishi maisha halisi" - Gaucho.

Muhtasari

• Unataka kunyanyasa hawa watu wametoka ghetto. Badala nyinyi ndio mnafaa kupeleka mswada bunge kuwatetea…” alisema.

 

Gaucho amkosoa vikali Jalang'o kwa kutowatetea wanablogu.
Gaucho amkosoa vikali Jalang'o kwa kutowatetea wanablogu.
Image: Screengrab, Instageam

Mwanaharakati na rais wa bunge la wananchi Gaucho amemsuta vikali mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor katika kile alisema kwamba ameshindwa kuwatetea wakuza maudhui dhidi ya ushuru wa 15% unaopendekezwa na serikali ya Kenya K               wanza.

 Hii inakuja siku chache baada ya Jalang’o kupakia video kwenye Instagram yake akisema kuwa mikono yake imefungwa katika suala zima la kuwatetea wanablogu, ambapo yeye pia kwa wakati mmoja alikuwa mwanablogu.

Jalang’o alisema kuwa wanablogu hao ndio walijiingiza kwenye mtego wa kuonesha serikali kwamba wana hela ndefu kwa kupakia maisha ghali mitandaoni, jambo ambalo limevutia serikali kutaka kuwakata ushuru wa 15%.

Lakini Gaucho amemkosoa Jalang’o kwa matamshi haya akisema kuwa wanablogu wengi, kama ambavyo alikuwa yeye kabla ya kuwa mbunge, huwa wanaigiza maisha mitandaoni na Jalang’o mwenyewe anajua hilo, na hivyo anapaswa kuwatetea bungeni dhidi ya ushuru wa 15% unaopendekezwa na serikali.

“Jalang’o niliona akiongea mambo ya wakuza maudhui akisema kwamba yeye anaunga mkono. Hao wanablogu wengi wanaishi na balloon, wanaishi kwa hewa, wanafeki maisha. Kama Jalang’o tu alikuwa anafeki maisha, zamani mimi nilikuwa najua Jalang’o alikuwa na pesa. Wakati alisimama MP Lang’ata ndio nilijua hakuwa na pesa, alikuwa na pesa tu ya kula hata gari alikuwa anapiga tu PR. Na hiyo ndio kitu inafanyika na wakuza maudhui wengine,” Gaucho alisema.

Kulingana na rais huyo wa bunge la wananchi, Jalang’o ni kama amesahau alikotoka na sasa kwa sababu ni mbunge ,amesahau kuwa wanablogu wengi ni walala hoi ambao wanafaa kutetewa dhidi ya pendekezo la ushuru wa 15%.

“Wewe ukikuja kwanza sasa hivi unakula pesa bure, surely Jalang’o, unasahau mahali umetoka, mahali pa kufeki maisha sasa hivi unaishi maisha halisi, unataka kunyanyasa hawa watu wametoka ghetto. Badala nyinyi ndio mnafaa kupeleka mswada bunge kuwatetea…” alisema.

Katika mswada wa fedha wa 2023, serikali imependekeza miongozi mwa tozo nyingine nyingi, kutozwa ushuru wa 15% kwa wanablogu wa mitandaoni ili kuchangia katika mfuko wa kitaifa wa serikali kusukumu bajeti ya mwaka 2023-24.