Wengi maisha imewaendea mrama-Njugush azungumzia ushuru wa asilimia 15 kwa waunda maudhui

Njugush anasema kuwa ingawa ni wajibu wa serikali kukusanya mapato, kuna haja ya miundo sahihi ambayo haitishii kazi za waunda maudhui.

Muhtasari
  • Njugush anasema kuwa ingawa ni wajibu wa serikali kukusanya mapato, kuna haja ya miundo sahihi ambayo haitishii kazi za waunda maudhui.
Mchekeshaji Timothy almaarufu Njugush
Mchekeshaji Timothy almaarufu Njugush
Image: INSTAGRAM

Mcheshi Timothy Kimani almaarufu Njugush ametaja pendekezo la serikali katika Mswada wa Fedha wa 2023 la kuwatoza ushuru waundaji wa maudhui ya kidijitali kwa asilimia 15 kuwa si sawa.

Njugush anasema kuwa ingawa ni wajibu wa serikali kukusanya mapato, kuna haja ya miundo sahihi ambayo haitishii kazi za waunda maudhui.

Katika mahojiano na Hot 96 FM siku ya Jumatatu, mcheshi huyo alikanusha simulizi kwamba waundaji wa maudhui wana pesa za kusawazisha, akisema baadhi yao wakati fulani wameamua kufadhili watu kwenye mitandao ya kijamii wanapokuwa na matatizo ya kifedha.

“Rais aliposema mimi na Butita tunapata pesa nyingi kuliko yeye, nilijua kuna tatizo, simulizi kwamba aliuza kwamba watengeneza maudhui wanapata pesa nyingi sana. Hata hivyo kwa upande wangu nahisi huo sio uungwana kwa sababu baadhi ya waunda maudhui niliona Jalang'o wanasema wengi tunaonesha magari lakini wakati huo huo hakutaja wengi tunaweka bili za kulipia maisha imewaendea mrama ," alisema.

Kulingana na Njugush, uundaji wa maudhui unaweza kuonekana kuwa wenye manufaa lakini serikali inajaribu kusimamia simulizi ili kukamua pesa zaidi kutoka kwa waundaji mtandaoni.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya waundaji wa maudhui ya kidijitali ambao hutengeneza maudhui kwa ajili ya kujifurahisha, bila faida, wakishangaa kama watahitajika pia kuwasilisha marejesho mwishoni mwa kila mwaka katika visa kama hivyo.

“Tax kulipa ni wajibu wa kila mtu na lazima tufanye hivyo ili nchi ikue, lakini shida yangu ni hawa watu walewale, unajua tunaigiza kama wamefika wameland kama captain Otoyo, wametua tu, hawa ni watu wale wale. alituahidi uwanja wa Kamarini kwa miezi sita kwa miezi sita mpaka miaka kumi ikapita na kamarini stadium bado haijakuja bado wataenda kumtoza mtu akishinda huko nje,” Njugush narrated.

Haya yanajiri baada ya mbunge wa Lang'ata kusema kwamba ana wakati mgumu wa kuwatetea waunda maudhui kwani wamekuwa wakipakia pesa na magari mitandaonin ili kuonyesha jinsib wako na pesa.