• Davido alifichua haya katika mahojiano na Podcast ya Million Dollar Worth Of Game, iliyochapishwa Jumatatu.
• "Watu wengi walidhani tutaangusha albamu na kutakuwa na huzuni nyingi, wanaume tuliwapa bangers baada ya bangers.” - Davido.
Mwimbaji nyota kutoka Nigeria, David Adeleke, almaarufu Davido, amesema kuwa ingawa watu walitarajia nyimbo nyingi za kusikitisha wakati albamu yake ya ‘Timeless’ ilipodondoka, aliimba vibao vyenye furaha na tafrija, kwa sababu alijua mama yake na mwanawe wanacheza mbinguni.
Davido alifichua haya katika mahojiano na Podcast ya Million Dollar Worth Of Game, iliyochapishwa Jumatatu.
Alisema, “Nilijitazama kwenye kioo nikasema, bruh, mbali na mimi kuwa juu yangu tu najua nina watu wengi wanaonipenda, watu wengi wanaonitegemea, mwanangu huko juu ananitazama, asingependa niwe kama mnyonge.”
Msanii huyo alisema kuwa ngoma nyingi alizoimba kwenye albamu hiyo ambayo aliitoa miezi michache kufuatia kifo cha mwanawe wa pekee,zilihimizwa na marehemu Ifeanyi, mwanawe kwaki anajua fika kwamba ana jukumu la kusimama upande wa faraja na mamake, ambaye ni mume wake na pia kuonesha dunia ujasiri wa kuweza kustahimili mambo magumu licha ya changamoto na mapigo kama hayo ya kufiwa.
"Mbali na mimi kuwa na nguvu kwa ajili ya mama yake, ambalo ni jukumu langu la msingi, lazima niwe na nguvu kwa ulimwengu.”
"Watu wengi walidhani tutaangusha albamu na kutakuwa na huzuni nyingi, wanaume tuliwapa bangers baada ya bangers.”
‘'Mwanangu anacheza, mama yangu anacheza mbinguni pia. Ili watu waone kuwa inawezekana. Sio kwamba ninamtakia mtu yeyote, singetamani kamwe kwa adui yangu, unaelewa?”
"Lakini kuweza kusimama tena na kuweza kufanya kazi. Ni Mungu tu, huwezi kuniambia chochote, ni Mungu tu.”Msanii huyo alimaliza kwa sauti iliyojawa na uchungu wa kiume.