Kwa nini Kaunda Suit za rais Ruto zimezua gumzo miongoni mwa Wakenya?

Ruto alionekana kwa mara ya kwanza akiwa amevalia Kaunda Suit Jumapili iliyopita katika ziara ya kiserikali nchini Djibout.

Muhtasari

• Nchini Djibout, Ruto alikuwa amevalia Kaunda Suit ya rangi ya samawati iliyokoza rangi akiwa na rais wa nchi hiyo Ismail Omar.

Rais Ruto azua gumzo na Kaunda Suit zake
Rais Ruto azua gumzo na Kaunda Suit zake
Image: Facebook

Rais wa Kwenya William Ruto ni mtu mmoja ambaye yuko makini sana muda wote ikija ni suala la kuchagua fasheni yake ya uvaaji.

Kwa muda wa wiki mbili sasa, mku wa taifa ameonekana akija fasheni tofauti kabisa ambayo imewaacha Wakenya katika gumzo kubwa.

Rais hivi majuzi ameanza kuboresha hali yake ya uanamitindo, akibadili kutoka kwa suti ya kawaida, rasmi zaidi na tai iliyo na blazi nyeusi na mashati meupe na tai nyekundu, hadi suti za Kaunda zisizo na rangi nyingi.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, Mkuu huyo wa nchi amegeuka vichwa baada ya kujitokeza hadharani akiwa amevalia suti hiyo ambayo inasemekana asili yake ilitoka Australia miaka ya 1970, lakini ilipata umaarufu zaidi barani Afrika na Rais wa kwanza wa Zambia, marehemu Kenneth Kaunda.

Rais Ruto alijitokeza kwa mara ya kwanza akiwa amevalia suti ya Kaunda wakati wa ziara ya Kiserikali nchini Djibouti mnamo Juni 11, 2023, na kuibua hisia tofauti kutoka kwa Wakenya mtandaoni katika mchakato huo.

Alipokutana na rais wa Djibout, Ismail Omar, akiwa amevalia suti hiyo ya Kaunda, wawili hao walijadili mengi ikiwemo ushirikiano wa mataifa haya mawili ambapo Kenya ingewapeleka walimu wa Kiingereza nchini humo kutoa mafunzo.

Wengi walidhani kwamba ilikuwa kaiwada tu ila Jumatano Ruto aliwafungua wengi midomo na kuanza kuongea, baada yake tena kuonekana na Kaunda nyingine katika mkutano wa nne wa makuzi ya maeneo ya mijini na  kongamano la Uhandisi mjini Naivasha.

Katika matukio hayo yote, Ruto alionekana amependeza ndani ya Kaunda Suit, kuwafanya baadhi ya Wakenya kwenye mtandao wa Twitter kuzua gumzo;

“Kwamba Rais William Ruto amekuwa mwana mtindo siku zote si jambo la shaka. Suti zake za Kaunda ni shwari,” mmoja alisema.

“Ruto na suti zake za Kaunda. WARDROBE ya Rais ni polepole kufanyiwa metamorphosis.” Mwingine alidakia.