Jacque Maribe aweka bayana uhusiano wake na Itumbi, Sam Oginna

Maribe aliweka wazi kwamba hajawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na yeyote kati ya wawili hao.

Muhtasari

• Maribe amejitokeza wazi na kuzungumzia uhusiano wake na waziri msaidizi katika wizara ya ICT Dennis Itumbi na mwanahabari wa zamani wa Citizen Tv, Sam Ogina.

• Maribe pia alizungumzia madai kwamba alimnyima anayedaiwa kuwa baba ya mtoto wake, Eric Omondi, fursa ya kumfanyia mtoto wao DNA.

Dennis Itumbi na Jacque Maribe.
Dennis Itumbi na Jacque Maribe.
Image: HISANI

Mwanahabari Jacque Maribe amejitokeza wazi na kuzungumzia uhusiano wake na waziri msaidizi katika wizara ya ICT Dennis Itumbi na mwanahabari wa zamani wa Citizen Tv, Sam Ogina.

Mama huyo wa mtoto mmoja alifafanua katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii kwamba hajawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na yeyote kati ya wawili hao.

Maribe pia alizungumzia madai kwamba alimnyima anayedaiwa kuwa baba ya mtoto wake, Eric Omondi, fursa ya kumfanyia mtoto wao DNA.

Maribe alisisitiza kwamba amekuwa na ushirikiano katika suala zima la kufanya uchunguzi wa baba halisi wa mtoto wake, akielezea masikitiko yake kwa kuhusishwa na mfanyikazi mwenzake wa zamani Sam Oginna kwenye gumvo hizi zinazoenea mitandaoni.

"Road trip ya kuponya akili na shukrani kwa marafiki wangu wenye akili timamu. Pia, wacha niweke kila kitu wazi. Muwache marafiki zangu. Je, ni vipi na kwa nini rafiki yangu Sam Ogina anaburutwa kwenye drama isiyomhusu? Hatujawahi kuchumbiana. Kama ulivyosema nilichumbiana na Dennis Itumbi. Niache,” Maribe alisema.

Mwanahabari huyo ambaye anakabiliwa na kesi mahakamani kwa madai ya kuhusika na kifo cha mfanyibiashara Monica Kimani wiki iliyopita alimkashifu Erick baada ya madai ya kuwa alikuwa ananyimwa nafasi ya kufanya DNA ili kubaini kama mtoto huyo ni wake. 

Mwezi Januari, Maribe, akionekana kuwa na mzaha, alimtambulisha Itumbi kama mkwe wa babake kwenye Instastory yake.

Alikuwa ameshiriki picha yenye nukuu ya Itumbi na babake.

"Bw Maribe na mkwe wake, haijalishi mtu yeyote atasema nini, tunasalia kuwa familia," alisema.