Lulu Hassan awashangaza wanamtandao baada ya kuonekana bila hijabu

Wanamtandao wengi walibaini kuwa ilikuwa mara ya kwanza kuona nywele zake.

Muhtasari

• Mtangazaji wa runinga Lulu Hassan amesifiwa kwa ustaarabu na adabu hata alipokuwa akihudumia mitindo ya urembo kwenye skrini na nje wakati wa hafla.

• Wengine walionekana kukasirishwa kwa kitendo hicho cha Lulu kutoa hijabu yake mbele ya watu ambayo haikubaliki kwa dini ya Uislamu, bali wengine walifurahishwa kwa kuona nywele yake Lulu kwa mara ya kwanza.

 

Lulu Hassan aonekana bila hijabu kwenye sherehe huku akimwagia bibi mkuu pesa
Lulu Hassan aonekana bila hijabu kwenye sherehe huku akimwagia bibi mkuu pesa
Image: Instagram

Mtangazaji wa runinga Lulu Hassan amesifiwa kwa ustaarabu na adabu hata alipokuwa akihudumia mitindo ya urembo kwenye skrini na nje wakati wa hafla.

Hata hivyo, video ya TikTok iliyopakiwa na @keahamani iliwafanya watu wafurahi kumuona akiwa mrembo wakati wa hafla iliyoonekana kama harusi.

Alivaa gauni refu jeupe lililofanana na vazi la harusi na kulipachika ua jekundu huku akisogea na rythym kwenye sherehe hiyo.

Kilichowashangaza watu wengi ni kwamba aliacha hijabu yake na kuonyesha nywele zake zilizosokotwa.

Wanamtandao wengi walibaini kuwa ilikuwa mara ya kwanza kuona nywele zake.

Lulu alicheza densi na bibi mkuu wa sherehe hiyo huku akimwekea pesa na waliohudhuria wakishangilia na kuimba ili aendelee.

Wakati fulani, alihama kutoka kwa bibi mkuu hadi kwa mwanamke mwingine huku akipiga densi ili kumpa pesa kutoka kwa bahasha kubwa.

Kitendo hicho kilizua gumzo baina ya wanamtandao kwani wanamtandao wengi walitoa maoni yao tofauti.

Wengine walionekana kukasirishwa kwa kitendo hicho cha Lulu kutoa hijabu yake mbele ya watu ambayo haikubaliki kwa dini ya Uislamu, bali wengine walifurahishwa kwa kuona nywele yake Lulu kwa mara ya kwanza.

"Ni nini kilikuwa cha maana kikakufanya uonyeshe nywele yako walai," alisema 

"Leo nimeona nywele yake kwa mara ya kwanza," Winniejohnsonjaber alisema.

"Lulu Hassan ni mrembo bila hijabu," Liznyarnyakach0 alisema kwa mbwembwe.

"Smart sana. Kwa nini uvae hijabu," user8329118362813 alisema.

"Bila hijabu Lulu ni kijana mrembo," cheeylotieno alisema.

"Lulu ni mrembo bila hijabu," dotti_eunice aliandika.

"Lulu ilikuwaje bila hijabu lakini umependeza sana," ambasa98 aliandika.

"Sasa kuja Citizen TV kutangaza habari bila hijab," colloarts254 alisema.

"Kumbe wanatoanga vitambaa kwa kichwa," perpsrugi8 aliandika.