RIP! Msanii wa Afrobeats kutoka Nigeria Wizkid amefiwa na mamake

WizKid mara nyingi amemtaja mama yake kama msukumo wake mkubwa na chanzo cha nguvu katika safari yake ya mafanikio. Alimlea WizKid na ndugu zake kama mama asiye na mwenzi.

Muhtasari

• Marehemu Bi. Balogun, alikuwa nguzo ya usaidizi katika taaluma ya muziki yenye mafanikio ya mwanawe

Wizkid afiwa na mamake
Wizkid afiwa na mamake
Image: Instagram, Twtter

Msanii maarufu wa hip-hop na wa kisasa wa Afrobeats, Ayodeji Balogun almaarufu Wizkid, alimpoteza mama yake, Jane Balogun siku ya Ijumaa.

Bi Jane Dolapo Balogun alifariki mwendo wa saa 1.30 asubuhi siku ya Ijumaa katika tukio la kushtua ambalo limeiweka tasnia ya burudani katika hali ya maombolezo.

Kifo cha Balogun kilithibitishwa na meneja wa msanii huyo, Sunday Aare, ambaye alisema mamake Wizkid alifariki asubuhi ya Ijumaa.

Marehemu Bi. Balogun, alikuwa nguzo ya usaidizi katika taaluma ya muziki yenye mafanikio ya mwanawe.

WizKid mara nyingi amemtaja mama yake kama msukumo wake mkubwa na chanzo cha nguvu katika safari yake ya mafanikio.

Marehemu anasemekana Alimlea WizKid na ndugu zake kama mama asiye na mwenzi, akionyesha ujasiri na uamuzi.

WizKid mara nyingi alionyesha upendo wake mkubwa na shukrani kwa mama yake katika muziki wake na taarifa za umma.