Kajala arudi kanisani na kutangaza kupata wokovu baada ya Harmonize kumuita tapeli

Katika picha ya pili, mlokole mpya wa mjini alipakia nukuu ya maandiko matakatifu kutoka kitabu ya Warumi.

Muhtasari

• “Uchungu ambao umekuwa ukipitia hauwezi kulinganishwa na furaha ambayo inakuja,” yalisema maandiko kaitka kitabu cha Warumi 8:18.

Kajala Masanja.
Kajala Masanja.
Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe Fridah Kajala Masanja ameamua kutafuta faraja ya wokovu kanisani wiki kadhaa baada ya aliyekuwa mpenzi wake Harmonize kuachia wimbo akisimulia makubwa jinsi Kajala na binti yake walimfanyia makuruhu na mapeto.

Wikendi iliyopita, Kajala aipakia picha akiwa katika vazi la heshima kabisa na mkononi amejihami na Biblia takatifu na kutangaza kwamba baada ya kuyatathmini maisha yake kwa muda, aliamua kumchaua Mungu na kumpa nafasi ya kwanza katika moyo wake, na wala si nafasi ya mwisho.

“Chagua Mungu kwanza, sio mwisho,” Kajala aliandika kwenye kapsheni.

Katika picha ya pili, mlokole mpya wa mjini alipakia nukuu ya maandiko matakatifu kutoka kitabu ya Warumi.

Katika kifungu hicho cha nukuu, Kajala alijiliwaza na maandiko kwamba uchungu ambao amekuwa akiupitia hauwezi fananishwa wala kulinganishwa na mazuri ambayo yatamfuata baada ya kumchagua Mungu Zaidi ya kitu kingine.

“Uchungu ambao umekuwa ukipitia hauwezi kulinganishwa na furaha ambayo inakuja,” yalisema maandiko kaitka kitabu cha Warumi 8:18.

Kwenye picha ya tatu, Kajala aliweka video akielekea katika maegesho ya magari huku akicheza wimbo wa Rose Muhando, Secret Agenda haswa kwenye sehemu ambayo Muhando anazungumzia kutopatikana na maadui zake.

Kajala baada ya kimya cha muda, amerejea ikiwa ni baada ya kuchafuana vikali na Harmonize mitandaoni.

Harmonize aliachia wimbo akisema kwamba Kajala – ambaye alikuwa mpenzi wake alishirikiana na binti yake Paula na kumtapeli kwa lengo la kumhamisha mjini lakini hawakufanikiwa ndio maana waliachana na yeye.