Diana Bahati afunguka kuhusu kero za mitandaoni kuhusu mwanaye Mogern

Nilipokutana na Bahati, tayari alikua amechukua watoto watatu, Purity,Morgan, na Rose. Wote walikuwa katika nyumba ya watoto.

Muhtasari

•Akizungumza na wasaidizi wake wa nyumbani katika kipindi cha mwingiliano cha YouTube,Diana alieleza kuwa hashangazwi na mambo ambayo watu wanayoyasema mitandanoni kuhusu mwanaye kwa sababu anaujua ukweli wake mwenyewe.

Diana Marua/Instagram
Diana Marua/Instagram

Mkuza maudhui na mshawishi Diana Marua Bahati,amezungumza kuhusu changamoto anazokabiliana nazo mitandaondi kuhusu mwanaye mkubwa Morgan ambaye alimuasili miaka kadhaa iliyopita.

Akizungumza na wasaidizi wake wa nyumbani katika kipindi kwenye  YouTube, Diana alieleza kuwa hashangazwi na mambo ambayo watu wanayoyasema mitandanoni kuhusu mwanaye kwa sababu anaujua ukweli wake mwenyewe.

Aesema kwamba si vibaya kutoa maoni na hisia kwani kila mtu ana haki ya kujieleza na kutoa hisia zake.

"Mengi yamesemwa,na silaumua vyombo vya habari,kila mmtu ana haki ya kutoa maoni yake,lakini najua ukweli wangu bila kujali wanachokisema watu." Alisema.

Alieleza kuwa mumewe Bahati alikuwa ameasili watoto watatu akiwemo Morgan kitambo kidogo kabla ya yeye na Bahati hawajaanza kuchumbiana.

"Nilipokutana na Bahati, tayari alikua amechukua watoto watatu, Purity,Morgan, na Rose. Wote walikuwa katika nyumba ya watoto. Morgan alikuwa amekuja kumuunga mkono Bahati katika moja ya hafla za tuzo,na alishinda moyo wa Bahati, na hivyo ndivyo Morgan alipokuja kuishi nasi.Alikuwa mtu wa kwanza kuniita mama, na ninashukururu milele kwa hilo."

Hata hivyo amesema kwamba huenda  kuwepo kwa mali yote wanayomiliki kwa sasa  imechangiwa na baraka za kuwaasili watoto hao ambao amewataja kuwa baraka kutoka kwa Mungu.

Aidha amewataja wanaomkera mitandaoni kuwa wanafiki ambao wanafanya kila juhudi kuirudisha familia yao nuyuma kwa kueneza uvumi za uhasama.

Alisema kwamba mti wenye matunda hurushwa mawe na hivyo ni njia moja ya kujenga kijamii,na kumfanya kuwa maarufu katika mitandai ya jamii.

Diana amewashauri watu wasisusie kuasili watoto na kuwalea kwa kuhofia maneno ya watu kwani mwisho wa siku utasaidia mtu kupata makazi. Kisema , Kero za mitandao zinaweka kukera lakini ni vyema kusimama na ukweli wako na kuyapuuza maneno ya watu