Karen Nyamu apakia video Samidoh akimpa maua, kumbato la kishua na mabusu moto

Samidoh alionekana akimlaki kwa kumbato la kishua mpenzi wake huku akimkabidhi koja la maua kabla ya kutia busu la moto kwenye midomo yake.

Muhtasari

• “Nilikuwa na wakati mzuri zaidi kwenye hii! Sydney Australia ilikuwa kitu kingine. Sikunasa dakika zote lakini hizi ni chache,” Nyamu alisema

Karen Nyamu na Samidoh.
Karen Nyamu na Samidoh.

Karen Nyamu haonekani kusahau hivi karibuni jinsi muda wake pamoja na mpenzi wake Samidoh ulivyokuwa nchini Australia siku chache zilizopita.

Video za Nyamu akijumuika na Samidoh jukwaani Australia zilivujishwa wiki mbili zilizopita, lakini mpaka sasa, seneta huyo maalum bado anazidi kuumbuka matukio muhimu kutoka kwa ziara hiyo.

Nyamu amepakia video fupi fupi zilizounganishwa na kuwa moja zikinasa matukio muhimu kwa haraka ambayo yalitokea nchini Australia na kuandika kapsheni kwamba ni moja ya ziara ambayo haitokuja kutoweka kwenye kichwa chake kwa jinsi alipata wakati murwa na baba wanawe.

“Nilikuwa na wakati mzuri zaidi kwenye hii! Sydney Australia ilikuwa kitu kingine. Sikunasa dakika zote lakini hizi ni chache,” Nyamu alisema akiwapa nafasi mashabiki wakec kujua ni kwa nini upendo wake na Samidoh unazidi kung’aa.

Katika moja ya klipu, Nyamu alionekana akiwa ndani ya ndege na baada ya kutua Sydney, alilakiwa na mpenzi wake Samidoh ambaye alikuwa ameenda huku siku chache kabla.

Samidoh alionekana akimlaki kwa kumbato la kishua mpenzi wake huku akimkabidhi koja la maua kabla ya kutia busu la moto kwenye midomo yake.

Nyamu anapakia hii video ikiwa ni siku chache baada ya kukiri kwamba hafurahii jinsi mke mwenza Edday Nderitu alivyofanya kwa kujiondoa kwenye uhusiano huo na kwenda Marekani.

Nyamu alisema kwamba atafanya kadri ya uwezo wake kuhakikisha kwamba Edday anarudi nyumbani ili kuendeleza nafasi yake kama mke wa kwanza kwa Samidoh, katika kile alichokisema kwamba hata Mungu hajakataza ndoa ya wake wengi kweney vitabu vyake vitakatifu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki wake kwenye video hiyo;

“Naomba siku moja nikutane na mtu ambaye atanipenda jinsi unavyompenda Samido. Mtu ambaye atafanya 90% ya kazi kwenye uhusiano...kazi yangu ikuwe ni kupokea mapenzi tu,” Martingila alisema.

“Aki iyo hug vile umeshikwa Ile kitu Mimi hunishika ni homa, stress na muscle pool” Karien Sharon.

“I watch more than 3 times 🥹🥹😍😍love is a beautiful thing 🤗🤗😍😍” Diva alisema.