Karen Nyamu afichua kinachomvutia kwa Samidoh na mbona hawezi kaa mbali naye

"Yule jamaa nampenda sana, anaweza kweli kweli. Ana talanta, roho nzuri, mkarimu sana kwa hiyo alinipenda nikawezwa. Nimefika,” Nyamu alisema.

Muhtasari

• Nyamu ni seneta Mteule na Samidoh kando na kuwa msanii ni afisa wa polisi nchini.

• Pamoja wana watoto wawili, lakini Nyamu ana mtoto mwingine na jamaa mwingine.

 

Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Samidoh na mpenziwe Karen Nyamu
Image: Maktaba

Seneta maalum Karen Nyamu kwa mara ya kwanza amewajibu wale ambao wamekuwa wakimkosoa kwa kumfuata mpenzi wake Samidoh kila sehemu anakoenda ndani na nje ya nchi.

Nyamu aliyasema haya katika mahojiano ya kipekee kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini ambapo alikiri waziwazi kwamba mapenzi yake kwa Samidoh hayatokuja kupungua wala kufifia.

“Samidoh ni baba kwa watoto wangu, ni msanii mkubwa Kenya kwani mbona nisiwe shabiki wake namba moja. Yule jamaa nampenda sana, anaweza kweli kweli. Ana talanta, roho nzuri, mkarimu sana kwa hiyo alinipenda nikawezwa. Nimefika,” Nyamu alisema.

Alisema kwamba ziara ya wote kwenda Australia si kwamba alikuwa anamfuata bali ni kitu ambacho walikuwa wamekipanga kwa muda mrefu.

“Si kweli kwamba kila mahali akienda namfuata. Mwaka huu amefanya tour Uropa mwezi mzima mimi sikuwa, alikuwa Uchina mimi sikuwa, sasa kuna ubaya gani tukienda naye Australia? Kwani nimekosea nani? Tena hicho ni kitu ambacho tulikuwa tumepanga kwa muda mrefu. Si kitu kwamba kwa sababu alikuwa kule nikamfuata. Ni kitu tulipanga muda na visa zilipatikana kwa wakati mmoja na huo ndio pia muda mimi nilipata nafasi,” alisema.

Seneta Nyamu hata hivyo alifutilia mbali uwezekano wa kupata mtoto wa tatu  na Samidoh hivi karibuni akisema kwamba kwa sasa wamechukua mapumziko kidogo ili kila mmoja afanye kazi.

Nyamu ni seneta Mteule na Samidoh kando na kuwa msanii ni afisa wa polisi nchini.

Pamoja wana watoto wawili, lakini Nyamu ana mtoto mwingine na jamaa mwingine.