Familia ya Kim Kardashian yadokeza tu kwamba huenda akagombea urais siku moja

Khloe aliongeza kwa kukiri, ‘Ninahisi kama Kim anaweza kuniambia kesho anagombea Urais na mimi ni kama, “Sawa, msichana, fanya mambo yako.” Kwa Kim ni kama siku nyingine.'

Muhtasari

• Mwaka 2018, habari zake kudokeza uwezekano wa kuwania urais wa Marekani zilizagaa baada ya mahojiano yake kwenye runinga ya CNN.

Kim Kardashian
Kim Kardashian
Image: X

Familia ya mwanamitindo tajiri Zaidi duniani, Kim Kardashian imefichua kwamba mpenzi huyo wa zamani wa Kanye West siku moja atawania kiti cha urais wa Marekani.

Hii ni  baada ya Kardashian kuendeleza mchakato wake wa kuzuru magereza mbali mbali Marekani akiwalipia bondi wafungwa ambao wanazuiliwa rumande kwa kukosa mdhamana.

Dadake Khloe Kardashian ambaye waliandamana naye kwa mujibu wa Daily Mail aliwaambia wanahabari kwamab licha ya kuwa dadake anafanya kwa roho safi tu lakini wakati utafika atapata msukumo wa kufanya Zaidi akiwa katika nafasi nzuri, na nafasi hiyo ya kuwatetea wafungwa wanyonge wa sheria ni kupitia yeye kuwa rais wa kuleta mageuzi na mabadiliko chanya katika mifumo ya kimahakama.

Khloe aliongeza kwa kukiri, ‘Ninahisi kama Kim anaweza kuniambia kesho anagombea Urais na mimi ni kama, “Sawa, msichana, fanya mambo yako.” Kwa Kim ni kama siku nyingine.'

Hii si mara ya kwanza kwa mrembo huyo kuweka kwenye mizani suala au azma yake kuwania urais wakati mmoja.

Mwaka 2018, habari zake kudokeza uwezekano wa kuwania urais wa Marekani zilizagaa baada ya mahojiano yake kwenye runinga ya CNN.

“Kusema kweli sidhani hilo liko akilini mwangu,” Kardashian alisema, akijibu swali la mtangazaji kuhusu iwapo angefikiria kugombea kama rais.

Hata hivyo, wakati mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo ya kisiasa alipomkumbusha Kardashian kwamba “[Donald] Trump ni rais, inaweza kutokea,” alijibu: “Najua, ndiyo maana [mume wangu] Kanye [West] – kipindi hicho - anampenda. Ni wazo kwamba chochote kinaweza kutokea."

Ingawa mwandishi huyo wa kitabu cha Selfish alibaini kwamba hapaswi "kamwe kusema kamwe" linapokuja suala la kuchukua jukumu la kisiasa, pia alifichua kwamba "sio kile ninachoenda."