Harmonize: Nimekuwa mtu mzima sasa na nimeacha utoto, nitampigia simu Diamond

" Ipo siku moja tu, ndio maana nasema tunakua kila siku, unajua kila siku unakuwa na mawazo mapya. Ipo siku, huwezi jua, nitafika niseme unajua lazima nimtafute kwa simu." Harmonize.

Muhtasari

• Hii ni kauli ya pili ndani ya siku mbili ambayo Harmonize ametoa akirejela kulegeza misimamo yake na aliyekuwa bosi wake wa zamani WCB Wasafi.

•  Juzi baada ya kushuka uwanja wa ndege, Harmonize alimshukuru Diamond kwa kumhongera baada ya kushinda mataji matatu nchini Marekani.

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Screengrabs: YouTube

Kwa mara ya kwanza msanii Harmonize amethibitisha kwamba anafikiria siku moja kupigia simu aliyekuwa baba yake wa Sanaa Diamond Platnumz akidai kwamba kilichowakosanisha ni utoto tu.

Akizungumza katka kituo cha Clouds, Harmonize alisema kwamba utoto ndio ulikuwa unawasumbua na anaamini hata Diamnd kuna muda atafika tu afikirie na kumtafuta kwa njia ya simu ili kunyoosha ubaya ulioko kati yao tangu mwaka 2019.

“Mimi sina tatizo na mtu yeyote, na sina tatizo pia na yeye [Diamond]. Kwa hiyo tukue tu kwa pamoja tujitambue tujua kwamba kabisa tushakuwa watu wazima. Ipo siku moja tu, ndio maana nasema tunakua kila siku, unajua kila siku unakuwa na mawazo mapya. Ipo siku, huwezi jua, nitafika niseme unajua lazima nimtafute kwa simu. Au yeye pia atakua aone kabisa lazima nimtafute ndugu yangu, ishaallah,” Harmonize alisema.

Hii ni kauli ya pili ndani ya siku mbili ambayo Harmonize ametoa akirejela kulegeza misimamo yake na aliyekuwa bosi wake wa zamani WCB Wasafi.

 Juzi baada ya kushuka uwanja wa ndege, Harmonize alimshukuru Diamond kwa kumhongera baada ya kushinda mataji matatu nchini Marekani.

Harmonize alisema kwamba kwa kitendo cha Diamond kumhongera, maanake ameshajitambua na hiyo ndio njia sahihi ya kuweza kusogeza tasnia ya Sanaa ya Bongo Fleva mbele pamoja.

Harmonize wikendi hii anatarajia kuzindua albamu yake ya Visit Bongo na tayari ameonesha kuvuta zogo lililokuwepo baina yake na Rayvanny.