Koffi Olomide kuachia kolabo kubwa na Davido Jumamosi hii mbele ya ujio wake Kenya

Bila shaka haya ni baadhi ya maandalizi yake makubwa kuelekea tamasha lake nchini Kenya ambalo limedhaminiwa na Radio Africa Group ambalo litafanyika Desemba 9 katika uwanja wa ASK Dome.

Muhtasari

• Tamasha hilo kwa jina Peace Concert, ambalo Olomide amelichukulia kama njia moja ya kurudisha urafiki na uhusiano mwema na mashabiki.

Koffi Olomide na Davido
Koffi Olomide na Davido
Image: Facebook

Gwiji wa muda mrefu katika malimwengu wa muziki wa Rhumba kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide ametangaza jambo lake kubwa litakalotokea Jumamosi hii ya Desemba 2.

Olomide kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alichapisha tangazo kwamba ataachia kolabo kubwa na mfalme wa miziki ya Afrobeats kutokea Nigeria, Davido.

Olomide alitaja kolabo hiyo kuwa itakuwa kubwa Zaidi na ya kufunga mwaka 2023.

“Hii ni kolabo ya mwaka, Jumamosi saa mbili usiku,” Olomide aliandika.

Kolabo yake ya Davido si jambo geni kwani msanii huyo anayetajwa kuwa wa kizazi cha zamani amekuwa akiwashirikisha au kushirikishwa katika kazi za wasanii wa kizazi kipya kama njia moja ya kuji

Bila shaka haya ni baadhi ya maandalizi yake makubwa kuelekea tamasha lake nchini Kenya ambalo limedhaminiwa na Radio Africa Group.

Tamasha hilo kwa jina Peace Concert, ambalo Olomide amelichukulia kama njia moja ya kurudisha urafiki na uhusiano mwema kati yake na mashabiki wake wa Kenya kufuatia kisa cha aibu cha mwaka 2016, litafanyika katika uwanja wa ASK Dome jijini Nairobi Jumamosi ya Desemba 9.

Itakumbukwa huu utakuwa ujio wake wa kwanza kwa Zaidi ya miaka 7 tangia 2016 alipofutiwa visa ya kusafiri kuja nchini Kenya baada ya tukio hilo aliloonekana akimkwatua mcheza densi wake wa kike kwenye jukwaa.

Katika mahojiano ya kipekee kwa njia ya simu na stesheni ya Radio Jambo, Olomide alisema kwamba ana hamu kubwa ya kujumuika na mashabiki wake Kenya akiwataja kama ‘ndugu na dada zangu wa Kenya’ huku pia akiushukuru uongozi mpya wa Rais Ruto kwa kumrejeshea vibali vyote vya kusafiri Kenya bila tashwishi.

Bila shaka ukitaka kupata tikiti za tamasha hilo kubwa la Rhumba, fuata maelezo hapa chini;