Ruth K bado ni bestie tena kwa herufi kubwa na mimba ni yake peke yake tu! - Mulamwah

Alimtambulisha Ruth K mwezi Oktoba 2021 saa chache tu baada ya kuweka wazi kwamba yeye na mama mtoto wake Carrol Sonie wameachana.

Muhtasari

• Akizungumzia ziara yao ya wiki moja Diani, Mulamwah alisema kwamba mipango yao ilikuwa ni kwenda nje ya nchi.

Mulamwah na Ruth K
Mulamwah na Ruth K
Image: Facebook

Mchekeshaji Mulamwah anazidi kusisitiza kwamba hana uhusiano wa aina yoyote na Ruth K Zaidi ya urafiki wa karibu tu – Bestie.

Mulamwah ambaye alizungumza na waandishi wa habari pindi baada ya kurejea kutoka ziara ya kujivinjari na Ruth K, Diani kaunti ya Kwale alisisitiza kwamba bado hakuna kilichobadilika.

Mulamwah ambaye kwa muda mrefu amekuwa akificha uhusiano wao hivi majuzi waliweka wazi kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza na mwishoni mwa wiki jana walipakia picha katika uwanja wa ndege tayari kuondoka kwenda Pwani kupunga upepo.

Mchekeshaji huyo sasa amejitenga mbali na mimba hiyo akisema kwamba ni ya kwake Ruth K tu mwenyewe na kudai kwamba bado uhusiano wao hauendi Zaidi ya urafiki tu.

“Ruth K bado ni bestiee tena kwa herufi kubwa, ni Ruth K na hiyo ndio jina yake. Mimba ni yake tu,” Mulamwah alisema.

Akizungumzia ziara yao ya wiki moja Diani, Mulamwah alisema kwamba mipango yao ilikuwa ni kwenda nje ya nchi lakini akasema huko Diani hata kama walikwenda kujifurahisha bado ilikuwa ni sehemu ya kazi yao.

“Vacation ilikuwa vizuri, moja ya hisia nzuri. Nilikuwa nimechukua likizo ya wiki moja kutoka kazini na nikasema wacha niende nikajivinjari kidogo, sijawahi kuwa nam uda wangu mwenyewe kwa Zaidi ya miaka 4 ni kazi tu. Ilikuwa twende nje lakini sasa muda haukuwa upande wetu, tunatumai mwakani tutapata muda twende huko nje kwenye tulikuwa tunataka. Lakini ilikuwa ni eneo zuri la kufungua akili lakini bado sisi tulikuwa kazini,” Mulamwah alisema.

Mulamwah na Ruth K walitangaza habari za kutarajia mtoto siku chache tu baada ya kuonekana katika hafla ya kitamaduni ya kujitambulisha nyumbani kwa kina mpenzi wake.

Alimtambulisha Ruth K mwezi Oktoba 2021 saa chache tu baada ya kuweka wazi kwamba yeye na mama mtoto wake Carrol Sonie wameachana.

Hata hivyo, miezi kadhaa baadae, alikanusha kuwa Ruth K si mpenzi wake na kusema ni msanii tu aliyemsajili katika lebo yake ya Mulamwah Entertainment.