"Mungu alifanikisha!" Mulamwah na Ruth K waweka wazi kutarajia mtoto wao wa kwanza

Ruth K ameweka wazi kuwa na mimba siku chache tu baada ya kufanya sherehe ya kitamaduni ya kile kilionekana kama ni kumtambulisha Mulamwah kwa nasaba yake.

Muhtasari

• Takribani mwezi mmoja uliopita, wawili hao walifanya sherehe ya kitamadnuni nyumbani kwa kina mrembo ambapo walikuwa wamevalia mavazi yaliyorandana.

Mulamwah na Ruth K.
Mulamwah na Ruth K.
Image: Insta

Haitmaye Mulamwah na mpenzi wake Ruth K wameweka wazi picha za ujauzito mkubwa, wiki kadhaa baada ya kukanisha uwezekano wa kuwa na mimba.

Mulamwah na mpenzi wake ambaye bado anamrejelea kama rafiki wake tu walipakia picha yake akiwa na ujauzito mkubwa na katika chapisho lake, Mulamwah alisema kwamba yote ni mipango iliyoratibiwa na kufanikishwa na Mungu.

“Bestie, Mungu alifanikisha,” Mulamwah aliandika.

Ruth K naye alichapisha picha yoyo hiyo kwenye ukurasa wake na kusimulia jinsi alijipata amezama kwenye kina kirefu cha mapenzi yasiyojua kufa.

Ruth K alisema kwamba ulianza urafiki, mapenzi na kisha ujio wa maisha mapya, kwa maana kwamba sasa anatarajia kuitwa mama na kumpakata mwanawe kwa mara ya kwanza.

“Kwanza ulikuja upendo, upendo ambao uliumba maisha mapya, baraka ambayo hutujaza na furaha na furaha. Kuunda maisha ni hisia bora zaidi🤗❤️ kwamba tayari unapendwa. Siwezi kusubiri kukutana nawe,” Ruth K alisema.

Takribani mwezi mmoja uliopita, wawili hao walifanya sherehe ya kitamadnuni nyumbani kwa kina mrembo ambapo walikuwa wamevalia mavazi yaliyorandana.

Mulamwah baadae katika mahojiano na waandishi wa habari za mitandaoni, alikanusha kuwa haikuwa sherehe ya kuhusishwa na ndoa kwani alikwenda kwa kina Ruth K tu kuwasalimia kwa vile yeye pia alishawahi fika kwao.

Mulamwah akiulizwa kuhusu uwezekano wa mimba, alikataa suala hilo akisema kwamba kilichoonekana ni vazi tu la Ruth K ambalo pengine fundi alikuwa amelishona vibaya kutokana na haraka ya kulishona.

Lakini sasa ni wazi kwamba Ruth K anatarajia kupata mtoto na kwa asilimia kubwa wengi wanahisi kwamba Mulamwah ndiye mhusika mkuu wa ujauzito huo japo anazidi kukataa akisema kwamba Ruth K ana mtu wake na asingeweza kuingilia maneno ya kibinafsi ya watu.

Hongera Ruth K!