Eric Omondi: Mwanamume wa miaka 40 anafaa kuoa mwanamke wa miaka 24

"Mwanamke wa miaka 24 ni wa mwanamume wa miaka 40. Mimi ninependekeza uoe mwanamke ambaye ako na nusu ya umri wako, na ikienda sana awe na robo ya umri wako…." alisema Omondi.

Muhtasari

• Katika hilo, Omondi pia alishauri kwamba kama mwanamume huna kazi au pesa, epuka kabisa na suala la kufikiria mapenzi kwani hata kwenye Biblia imekatazwa.

Eric Omondi na mpenziwe Lynne.
Eric Omondi na mpenziwe Lynne.
Image: Facebook

Mchekeshaji ambaye pia ni mwanaharakati Eric Omondi ametetea uhusiano wake na mpenzi wake Lynne ambao umekuwa ukikosolewa kutokana na pengo kubwa baina ya umri wao.

Omondi kupitia Radio Jambo na Massawe Japanni, alisema kwamba yeye amemuacha mpenzi wake Lynne na umri wa miaka 20, na kuutetea uhusiano wao kama mmoja ambao utasimama imara kwa muda mrefu.

Baba huyo wa mtoto mmoja na Lynne alitetea pengo hilo kubwa kiumri baina yao akisema kwamba tafiti nyingi zinaonyesha mahusiano yenye pengo kubwa la kiumri yanadumu kuliko yale ya wapenzi walioko katika mabano sawa.

Omondi alichukua nafasi hiyo kuwausia wanaume kwamba wasijaribu kuchumbiana na warembo ambao wako kaitka mabano ya umri sawa, kwani hilo ni jaribio ambalo litafariki hata kabla ya kufika.

“Kaka usioe mwanamke ambaye yuko kwenye mabani ya umri mmoja na wewe kiumri, eti nyote mko katika miaka ya 20s, hiyo imekufa kabla ifike…” Omondi alisema.

Omondi alikuwa na sababu ya kushauri hivyo, akisema kwamba wanawake aghalabu hukua na kukomaa haraka kuliko wanaume.

Mwanaharakati huyo ambaye pia ameanza kufuata nyendo za kuingia kwenye siasa alisema kwamba mwanamke sahihi kwa mwanamume yeyote yule aliye na umri nusu ya umri wa mwanamume huyo.

“Wanawake huwa wanakomaa mapema na haraka, mwanamke wa miaka 24 ni wa mwanamume wa miaka 40. Mimi ninependekeza uoe mwanamke ambaye ako na nusu ya umri wako, na ikienda sana awe na robo ya umri wako…. Kama uko na miaka 30 achana na wanawake wa miaka 29 kuteremka hadi 20….” Omondi aliongeza.

Katika hilo, Omondi pia alishauri kwamba kama mwanamume huna kazi au pesa, epuka kabisa na suala la kufikiria mapenzi kwani hata kwenye Biblia imekatazwa.

“Kama huna kazi au pesa achana na kuchumbiana au hata kuoa, hiyo hata ni dhambi kwenye bibilia, usijaribu, hiyo mimi nakuambia kutoka kwa uzoefu wangu… tafuta pesa kwanza,” alishauri.