Nataka babe tukiachana kwa bus station anakimbiza gari niko ndani akilia - Samidoh

"Miaka ikisonga sasa sitaki mambo mob! Nataka babe tukiachana kwa bus station, anakimbiza hiyo mat niko ndani akilia😜" Samidoh alisema.

Muhtasari

• Tamko hili la utani lilijiri muda mchache baada ya kubainika kwamba msanii huyo yuko nchini Marekani kwa ajili ya kuitembelea familia yake.

Samidoh
Samidoh
Image: Facebook

Msanii wa Mugithi, Samidoh amefunguka kuhusu kile ambacho anakitaka katika maisha yake kuanzia sasa kwenda mbele, akisema kwamba amegundua miaka inazidi kumpa kisogo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook wikendi iliyopita, Samidoh aliandika kwamba amegundua miaka haipo upande wake na kusema kwamba kwa sasa hataki mambo mengi bali ni mwanamke wa kumpa mapenzi ya kweli.

Samidoh alisema kwamba anachokitaka sasa ni kuwa na mwanamke mwenye wakigombana kidogo wakiwa katika kituo cha magari ya abiria, basi mwanamke huyo anakimbia kwa miguu akifuata gari ambalo yeye ameliabiri huku akilia.

“Miaka ikisonga sasa sitaki mambo mob! Nataka babe tukiachana kwa bus station, anakimbiza hiyo mat niko ndani akilia😜” Samidoh alitania.

Tamko hili la utani lilijiri muda mchache baada ya kubainika kwamba msanii huyo yuko nchini Marekani kwa ajili ya kuitembelea familia yake.

Picha ziliibuliwa mitandaoni zikimuonyesha Samidoh akiwa na wanawe na mkewe Edday Nderitu katika jimbo la Boston nchini Marekani na kuzua gumzo pevu.

Itakumbukwa Edday Nderitu hivi majuzi alimzomea vikali Samidoh kwa kile alimtuhumu kumpeleka mpenzi wake Karen Nyamu katika nyumba ambayo alidai walishirikiana kujenga kijijini mwao.

Edday alisema kwamba kitendo hicho kilimkosea heshima akifichua kwamba Samidoh angeishia kuwaona wanao katika mitandao ya kijamii tu wala asingemruhusu kuwakaribia.

Lakini ilikuwa ni kinaya kuona Samidoh akikutana na watoto hao na hata kukumbatiana na kuashiria kwamba matamshi ya Edday yalichochea na pengine hasira tu.