Rapudo na Amber Ray waandaa tafrija ya kukata na shoka kuonesha sura ya mwanao

Tafrija hiyo ilikuwa ni mahususi kwa watu walioalikwa pekee na miongoni mwao ni crush wa Amber Ray, Oga Obinna.

Muhtasari

• Nyumba ilipambwa kwa waridi nyingi nyekundu, kamili na mandhari ya glasi iliyochorwa 'Africanah to the world'.

Kennedy Rapudo na Amber Ray
Kennedy Rapudo na Amber Ray
Image: Screengrab//tiktok

Mwanasosholaiti Amber Ray na mpenziwe ‘tajiri’ Kennedy Rapudo hatimaye wameonesha mashabiki wao sura ya binti yao Africanah kwa mara ya kwanza tangu azaliwe miezi kadhaa iliyopita.

Wawili hao ambao si wageni kwa kutanua vifua mitandaoni wakionesha wanavyovimiliki na maisha yao ya starehe waliandaa tafrija ya kukata na shoka kwa ajili ya binti yao.

Tafrija hiyo ilikuwa ni mahususi kwa watu walioalikwa pekee.

Itakumbukwa tangu mtoto huyo, Africanah, azaliwe mnamo Mei mwaka jana, wamekuwa wakimtaja tu jina lake na kuonyesha vitu ghali wanavyomnunulia lakini hawajawahi kuweka wazi sura ya uso wake.

Nyumba ilipambwa kwa waridi nyingi nyekundu, kamili na mandhari ya glasi iliyochorwa 'Africanah to the world'.

Pia kulikuwa na bar wazi na buffet. Video zinazosambaa mtandaoni zinaonyesha watu mashuhuri kadhaa, kama vile Oga Obinna, sosholaiti Risper Faith, Eric Omondi, miongoni mwa wengine, kwenye hafla hiyo ya kipekee.

Wote walikuwa katika maviazi meusi, wanaume wakiwa wamevalia suti na tuxedo, huku wanawake wakibinafsisha mavazi yao meusi katika muundo wa kipekee.

Video ya TikTok iliyoshirikiwa na @unnipraise ilionyesha wageni wakiwa wamekusanyika katika eneo la sebule chini ya ngazi, huku Amber na Rapudo wakiwa wamesimama juu, wakimuonyesha msichana wao mdogo kwa wageni.

Rapudo na Amber Ray licha ya kuonekana kuwa kamili kwa kila kitu mitandaoni, maisha yao ya ndoa yamekuwa ya visa na vitimbi huku wakiachana na kurudiana mara kwa mara.

Hata hivyo, mashabiki wao wengi hawajawahi amini iwapo wanaachana kweli ama ni mbinu zao za kuigiza mitandaoni kutafuta kiki.