Kanye amemtaka Kim kuwatoa watoto wao katika "shule bandia ya watu mashuhuri"

Wawili hao, ambao wametalikiana tangu 2021, wana watoto wanne: North West, 10, Saint West, 8, Chicago West, 6, Psalm West, 4.

Muhtasari

• Mnamo Septemba 2022, rapper huyo wa "All of the Lights" alisema yeye na Kardashian walikuwa na "mazungumzo mazuri" kuhusu elimu ya watoto wao.

kanye West na familia yake.
kanye West na familia yake.
Image: BBC News

Kanye West amemtaka mke wake wa zamani Kim Kardashian hadharani kuwatoa watoto wao katika "shule bandia ya watu mashuhuri."

Wawili hao, ambao wametalikiana tangu 2021, wana watoto wanne: North West, 10, Saint West, 8, Chicago West, 6, Psalm West, 4.

Tangu kutengana kwao, wawili hao wamekuwa wakizozana kuhusu jinsi ya kulea watoto wao.

“Kim waondoeni wanangu katika shule ya Sierra Canyon sasa, hiyo ni shule ya feki ya watu mashuhuri ambayo inatumiwa na ‘system’” rapper huyo aliandika kwenye kurasa wa Instagram Jumatano usiku.

Alinukuu chapisho hilo la kushangaza, "Kwa wakati huu kila mtu anajua 'system' ni neno la msimbo la nini. Niliondolewa kutoka kwa baba yangu na system, na system iliniondoa kutoka kwa watoto wangu.

"System inapoandaa wanamichezo, wanaepuka kufanya kazi na wale ambao wana baba zao maishani kwa sababu ni ngumu kuwadhibiti."

“Wanangu wawili wakubwa wanajua baba yao," msanii wa hit wa "All Falls Down" aliongeza.

Watoto hao wanne wanahudhuria Shule ya Sierra Canyon kwa muda wote na kisha wanafanya shughuli za ziada katika shule ya Donda West - shule ya kibinafsi ya Kikristo iliyofunguliwa na rapa huyo mwaka wa 2022 na iliyopewa jina la marehemu mamake Donda West.

Ingawa YE hawezi kukubaliana na mbinu zote za uzazi za Kardashian, hapo awali alikiri kwamba mwanzilishi wa Skims ana watoto wao "asilimia 80 ya muda."

Mnamo Septemba 2022, rapper huyo wa "All of the Lights" alisema yeye na Kardashian walikuwa na "mazungumzo mazuri" kuhusu elimu ya watoto wao.

Walakini, inaonekana kwamba njia yoyote ambayo wapendanao hao wa zamani walikuwa wameifanya imefikia mwisho, kama West alimwambia Tucker Carlson kwamba hayuko tayari "kupindisha" linapokuja suala la elimu.