Betty Kyallo atangaza kuonyesha picha zake akiwa na bikini, ‘ficheni simu za watoto wenu!’

Kyallo aliwataka wazazi kuficha simu za wanao mbali kabisa kwani hivi karibuni ataanza kupakia picha zake akiwa kwenye bikini, jambo ambalo hataki watoto chini ya umri wa miaka 18 kuona

Muhtasari

• Hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja hajawahi weka wazi kama yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi au la.

Betty Kyallo.
Betty Kyallo.
Image: Instagram

Mwanahabari Betty Kyallo amewatahadharisha wazazi kuficha simu za watoto wao wakni ana jambo jipya ambalo asingetaka liwaharibu watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18.

Kupitia Instagram yake, Betty ambaye alikuwa anasherehekea umri wa miaka 35 alijisherehekea na kufichua kwamba hivi karibuni atarejelea kupiga picha akiwa amevalia vazi aina ya bikini.

Mrembo huyo mama wa mtoto mmoja alisema kwamba kwa ajili ya hilo, angewataka wazazi waweke mbali simu za watoto wao wasije wakaona wasiyostahili kuona mitandaoni.

“Heri ya kuzaliwa kwangu. Inaonekana moto zaidi kuliko wabaya wako. 😂😂😂 pia ninakaribia kuvaa bikini zangu. Chukua simu ya watoto wako😂😂 kwaheri,” Betty Kyallo alisema.

Kyallo amekuwa mkimya katika mitandao ya kijamii katka miaka ya hivi karibuni lakini jana akisherehekea siku yake ya kuzaliwa alitangaza kwamba anakuja na mwamko mpya, lakini akatoa angalizo hilo kwa wazazi.

Hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja hajawahi weka wazi kama yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi au la.

Hii ni licha ya kutoka na msanii Stevo Simple Boy na kwenda kwenye date wiki mbili zilizopita.

 Katika picha zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii, Stevo na Kyallo walionekana nadhifu kwenye mtoko wa jioni wakila pamoja kwenye meza moja.

Baadae Stevo alifichua kwamba walizungumzia mengi kuhusu maisha yao ya kimapenzi, Kyallo akimuahidi kumpa jibu la kuridhisha wakati watakutana tena.