“Starehe yangu kubwa ni wanawake!” Dulla Makabila afichua baada ya Manara kuoa mpenziwe

"Mimi kwanza situmii chochote; sivuti sigara, bangi, pombe, sitazami filamu wala kuvuta shisha. Hata mpira siangalii. Mimi napenda play station na madem. Ndio vitu vyangu hivyo,” alisema.

Muhtasari

• Itakumbukwa miezi michache iliyopita, msanii huyo alikuwa kweney vyombo vya habari baada ya Haji Manara kudaiwa kumchukulia mke wake.

Dulla Makabila
Dulla Makabila
Image: Instagram

Msanii wa muziki aina ya Singeli kutoka Bongo, Dulla Makabila amefunguka ukweli wake kwamba starehe yake kubwa huipata kwa warembo wala si kwa vitu vingine ambavyo wanaume wengi wanavipenda.

Akizungumza kwenye Wasafi FM, Makabila alisema kwamba asingependa kuwa muongo kwani ukweli wake ni kwamba yeye ni mraibu wa Kamari, pombe wala kutazama filamu na michezo mingine, bali muda wake wa kustarehe hutumika vizuri akiwa na warembo.

“[Kupenda warembo] ndio utaratibu wangu wa kila siku. Mimi kwanza situmii chochote; sivuti sigara, bangi, pombe, sitazami filamu wala kuvuta shisha. Hata mpira siangalii. Mimi napenda play station na madem. Ndio vitu vyangu hivyo,” Makabila alisema.

Msanii huyo aliweka wazi kwamba yeye asingependa kuwa muongo na kama mtu anataka kumkosea kabisa wasiwahi zungumza maisha, basi cheza na mpenzi wake.

Itakumbukwa miezi michache iliyopita, msanii huyo alikuwa kweney vyombo vya habari baada ya Haji Manara kudaiwa kumchukulia mke wake.

Haji Manara alifunga harusi na mrembo muigizaji kwa jina Zaylissa ambaye alitajwa kuwa ni mpenzi wa Dulla Makabila.

Baadae msanii huyo aliachia wimbo wenye hisia kali akiwazomea na kuwatolea uvivu Manara na Zaylissa jambo ambalo lilifika mikononi mwa polisi na kutakiwa kufika kituoni kurekodi taarifa.

Hata hivyo, alipoulizwa kama wanazungumza na Manara, Makabila alikataa kabisa kulizungumzia hilo akisema “achana na hayo mambo.”

Hii hapa ni video yake akifichua ukweli wa kile anachokipenda.