Wasanii wa Tanzania kitu wananishinda ni kuimba kama ndege lakini kifedha hawanifikii - KRG

"Sikuwa najua mimi ni mkubwa sana Tanzania hata kuliko hapa Kenya, kusema ukweli. Tanzania mimi ni Bughaa sasa," alisema.

Muhtasari

• Kwa kustaajabishwa, KRG amefichua kwamba alipata ana mashabiki wengi sana nchini Tanzania kuliko hata nyumbani kwao Kenya.

KRG.
KRG.
Image: Facebook

KRG the Don ameweka wazi kiini cha ziara yake katka nchi jirani ya Tanzania wiki jana.

Kando na kwenda kumuonyesha uungwaji mkono msanii Alikiba katika hafla yake ya kuzindua kituo chake cha runinga ya redio, KRG amefichua kwamba kikibwa kilichompeleka kule ni kujumuika na mashabiki wake.

Kwa kustaajabishwa, KRG amefichua kwamba alipata ana mashabiki wengi sana nchini Tanzania kuliko hata nyumbani kwao Kenya.

“Kitu kingine mimi nilienda pale kujumuika na mashabiki wangu, kwa sababu nina mashabiki wengi sana kupitiliza. Sikuwa najua mimi ni mkubwa sana Tanzania hata kuliko hapa Kenya, kusema ukweli. Tanzania mimi ni Bughaa sasa, nyinyi mnacheza na Bughaa… kule mimi ni mkubwa kuliko wasanii wao wote ukiwajumuisha nawashinda kwa kila kitu.”

“Labda ile kitu wananishinda ni kuimba kama ndege, hiyo niliwaambia hiyo wananishinda roho safi lakini kwa kutafuta hela, hata nikilala kwa miaka 10 sidhani kama kuna wasanii watanifikia mimi,” KRG aliongeza.

Mapema wiki hii baada ya kurejea kutoka Tanzania, KRG alidhihaki taifa hilo akisema kwamba uchumi wa taifa zima haufikii uchumi wa jiji la Nairobi pekee.

“GDP ya Nairobi, pesa inazunguka tu Nairobi pekee, hata Tanzania nchi nzima haiwezi fika. Hiyo ni siri nimewaambia ambayo hamkuwa mnajua. Halafu ucheze na Wakenya wewe? Mimi naweza nunua Tanzania wasanii wao wote kutoka Diamond mpaka yule anatokea leo wakishikanishwa, wote nawanunua na nawaambia ni Bughaa,” KRG alijipiga kifua.