Zari afichua kazi maalum anayofanya Shakib kando na kuandamana naye kila mahali

"Watu wengi hawajui kazi yake, yeye huwa hafunzi watu kweney gym, ni mfanyibiashara wa magari,” Zari alieleza.

Muhtasari

• Wengi wamekuwa wakidhani kwamba Shakib hana kazi malum Zaidi ya kuongozana na Zari katika kila shughuli na kila sehemu mfanyibiashara huyo anakokwenda.

Zari na Shakib
Zari na Shakib
Image: Screengrab, Instagram

Kwa mara ya kwanza, mwanasosholaiti kutoka Uganda Zari Hassan ameweka wazi kazi maalum ambayo mpenzi wake Shakib Cham anajishughulisha nayo.

Wengi wamekuwa wakidhani kwamba Shakib hana kazi malum Zaidi ya kuongozana na Zari katika kila shughuli na kila sehemu mfanyibiashara huyo anakokwenda.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano nchini Tanzania, Zari alikanusha madai hayo akisema kwamba mumewe ana kazi maalum ambayo anaifanya, lakini hapendi kuiweka mitandaoni.

Alikanusha kwamba anamfungia sana kwa kumfanya kuwa kama mlinzi wake kumfuata kila sehemu bila kuzungumza neno lolote na waandishi wa habari.

“Ukiangalia vizuri mimi natembea na mume wangu, yeye ndiye rafiki yangu, ndiye mtu wangu wa karibu na pia ni mwambata wangu katika mapenzi, ananisapoti katika kila kitu nafanya na hilo ndilo linanifanya namdhamini sana.”

“Ana kazi zake, mume wangu ni mfanyibiashara, kwani mnadhani mimi pia ninavyozunguka sina kazi Afrika Kusini? Lazima tukitembea na mume wangu nina kazi pia ninaziacha. Mume wangu kazi yake kwanza anauza magari, watu wengi hawajui kazi yake, yeye huwa hafunzi watu kweney gym, ni mfanyibiashara wa magari,” Zari alieleza.

Awali, mama huyo wa watoto 5 alifichua furaha katika ndoa yake kukolea baada ya wanandoa hao kurejea kutoka Umrah nchini Saudi Arabia ambako walikwenda mwanzo mwa mwezi Machi.