MP Peter Salasya aorodhesha sifa za mwanamke anayetaka kumuoa

“Nataka kuoa lakini sitaki mwanamke mwenye atanikalia chapati. Aniruhusu niwe naye mara moja tu kwa mwezi. Apende kukaa kijijini kuliko Nairobi..." Salasya alidokeza.

Muhtasari

• Aliwaomba wafuasi wake kumpa ushauri ama aoe mwaka huu au mwaka kesho.

PETER SALASYA
PETER SALASYA
Image: FACEBOOK

Mbunge wa Mumias ya Mashariki, Peter Salasya ameweka wazi kwamba yuko sokoni na anatafuta mwanamke wa kufunga ndoa naye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Salasya alifichua kwamba amechoka kukaa mseja na anahitaji mwanamke mzuri wa kukaa naye katika ndoa, kwani maisha bila mke yanampa uhuru mwingi usio na tija katika maisha yake.

Aliwaomba wafuasi wake kumpa ushauri ama aoe mwaka huu au mwaka kesho.

“Je, nioe mwaka huu au mwaka ujao? Naomba unishauri. Nataka kuwa serious na maisha. Hii life bila wife inanipa uhuru sana ambao hauhitajiki sana,” Salasya alisema huku akionesha picha akiwa amebarizi kwenye kochi la kifahari nyumbani kwake.

Salasya alisonga mbele na kutaja baadhi ya vigezo na sifa ambazo anahitaji kutoka kwa mwanamke anayetaka kumuoa.

Salasya alisema kwamba hataki mwanamke anayekuja kwake na kuanza kumuongoza katika kila maamuzi na pia akaweka wazi kwamba anataka mwanamke ambaye atakubali kuishi kijijini kwao na wanaonana mara moja tu kwa mwaka.

“Nataka kuoa lakini sitaki mwanamke mwenye atanikalia chapati. Aniruhusu niwe naye mara moja tu kwa mwezi. Apende kukaa kijijini kuliko Nairobi. Naeza pata kweli?” Salasya aliuliza.

Mbunge huyo mseja tangu achaguliwe katika uchaguzi amekuwa akidokeza kutafuta mke.