'Wewe ni zawadi ya thamani zaidi ambayo Mungu alitupa' - Edday akimsherehekea bintiye

“Ninaposherehekea Siku yako ya Kuzaliwa, naomba Mungu akubariki na afya njema, akulinde na yule mwovu, utononoke na kung'aa milele kama nyota ...” aliongeza.

Muhtasari

• Edday alihamia Marekani na wanawe 3 takribani mwaka mmoja uliopita baada ya kudai kuyumba kwa ndoa yake ya miaka 15 na msanii wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi, Samidoh.

EDDAY NDEIRTU NA BINTIYE
EDDAY NDEIRTU NA BINTIYE
Image: FACEBOOK

Edday Nderitu, mpenzi wa Samidoh anayetajwa kuwa mama wa nguvu amemshereheka bintiye mdogo Nimo Muchoki anapofikisha miaka miwili tangu kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Edday alimtungia ujumbe mzuri na maalum bintiye akisema kwamba ujio wake duniani ni moja ya zawadi yenye thamani ya hadhi iliyotukuka ambayo walipata wao kama wazazi, Edday na Samidoh.

“Siku kama ya leo miaka 2 iliyopita, Mungu alitubariki na binti mdogo mtamu @nimu_muchoki, wewe ni zawadi ya thamani zaidi ambayo Mungu alitupa,” Edday Nderitu aliandika.

Alimtakia maisha marefu, afya njema na kukua ili kuja kutawala kila kitu cha ndoto zake za utotoni.

“Ninaposherehekea Siku yako ya Kuzaliwa, naomba Mungu akubariki na afya njema, akulinde na yule mwovu, utononoke na kung'aa milele kama nyota ...” aliongeza.

Edday alihamia Marekani na wanawe 3 takribani mwaka mmoja uliopita baada ya kudai kuyumba kwa ndoa yake ya miaka 15 na msanii wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi, Samidoh.

Edday katika ujumbe mrefu aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook kipindi hicho, alisikitika kwamba hatoendelea kukaa na Samidoh iwapo msanii huyo bado ako katika mahusiano mengine na mwanasiasa Karen Nyamu.

Baada ya kutua Marekani na kufanikiwa kuwaingiza wanawe katika shule kwenye mfumo wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa Zaidi duniani, alifichua sababu iliyomfanya kuondoka na wanawe wote.

Kwa maneno yake, Edday alisema kwamba alitaka kumlinda kisaikolojia binti yao mkubwa ambaye tayari ako katika umri wa balehe dhidi ya sarakasi ambazo zilikuwa zinajitokeza mara kwa mara baina yake, Samidoh na Karen Nyamu.

Alisema kwamba asingetaka binti yao ambaye amefika umri wa kujitambua kushuhudia hayo yote na hivyo alichagua Amani ya nafsi yake kumpeleka mbali na sarakasi hizo ambazo bila shaka zingeleta athari hasi kwa maisha ya mbeleni ya binti huyo haswa katika dhana kuhusu wazazi wake.