Esther Musila aeleza jinsi anakabiliana na maneno ya watu mitandaoni kuhusu ndoa na Guardian Angel

"Pia huwa siangalii kile ambacho watu wengine wanafanya, ninaamini katika uhusiano wa kwangu, sitaki kuiga ya watu kwa vile nimezingatia sana katika upande wa kwangu,” Musila alimjibu mumewe aliyemuuliza swali hilo.

Muhtasari

• Lakini baada ya kujua kwamba hayo ndiyo maisha atakayoishi na mumew, alilazimika kuzoea na muda wote anaishi kama hajui iwapo kuna watu wanamsimanga mitandaoni.

 

Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Image: YouTube

Esther Musila, mke wa msanii Guardian Angel amefunguka mbinu ambazo amekuwa akizitumia kushinda majaribu na maneno yasiyo na tija ya watu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ndoa yake.

Akizungumza kwenye podiaskti ya pamoja na mumewe wa jina Love Wins, Musila alisema kwamba mwanzoni ilimkalia ngumu kwa vile hakuwa amezoea maisha ya kuchambuliwa mitandaoni.

Lakini baada ya kujua kwamba hayo ndiyo maisha atakayoishi na mumew, alilazimika kuzoea na muda wote anaishi kama hajui iwapo kuna watu wanamsimanga mitandaoni.

“Kwangu mimi nafikiri kitu kimoja ni kwamba muda wote niko kwenye anga zangu tu, huwa nachunga sana nafasi yangu, hiyo ni ya kwanza. Pia huwa siangalii kile ambacho watu wengine wanafanya, ninaamini katika uhusiano wa kwangu, sitaki kuiga ya watu kwa vile nimezingatia sana katika upande wa kwangu,” Musila alimjibu mumewe aliyemuuliza swali hilo.

“Mimi huwa naangalia tu lakini sina haja ya kujibu. Unajua mwanzoni ilikuwa ngumu kwangu kwa sababu sikuwa katika mitandao ya kijamii, na nilikuja katika sehemu hii ambayo naweza nikasema ni mbaya kwa kuwa kila mtu anafikiri ana nafasi ya kukuongoza nini cha kufanya, kuvaa, kula, unajua… kwa hiyo nimejifunza kwamba katika akili yangu nimeweka nadhiri kwamba ninapuuzilia mbali yote haya,” alimaliza.