Pasta Kanyari ataka kuondoka TikTok baada ya kukutana na Mpenzi Chokuu (video)

“Hii tiktok tulisema tutabanana sote, mapasta, mal**a, wote tutabanana hapa hapa. Usiondoke mchungaji. Mimi nimekwambia naitwa chapati pendua,” Chokuu alimwambia Kanyari huku akikiri kuwa shoga.

Muhtasari

• Mpenzi Chokuu alikiri kwa mchungaji kuwa yeye ni shoga na anapenda wanaume kauli iliyomshtua Zaidi Kanyari.

 
• Kwa kujiamini, Chokuu alitoa ungamo lake kwa pasta Kanyari kwamba anapenda wanaume na hakuna kinachoweza kubadilisha hilo hata maombi.

Pasta Kanyari na Mpenzi Chokuu
Pasta Kanyari na Mpenzi Chokuu
Image: Maktaba, Instagram

Mchungaji Victor Kanyari ameonyesha wasiwasi wake kwenye mtandao wa video fupi, TikTok baada ya kukutana na mwanachama wa LGBTQ anayeishi Ujerumani, Mpenzi Chokuu.

Kanyari katika kipindi chake cha mubashara kweney mtandao huo ambao amejiunga siku si nyingi zimepita, alipata ombi la Chokuu akitaka kujiunga naye.

Kanyari alimkubalia na baada ya kuona picha yake, alionekana kujuta akijiuliza maswali ya balagha kuhusu sehemu ambayo amejikuta na hata kutishia kuhama katika mtandao huo.

“Mungu wangu, Leo nimekutana na nani jameni. Nimekutana na watu wengi lakini Sasa hii, Mimi nitatoka tiktok Chokuu. Mimi nitahama tiktok watu walikuwa wananiambia nitoke. Yale mambo mnaongea ni makubwa,” Kanyari alisema.

Mpenzi Chokuu alikiri kwa mchungaji kuwa yeye ni shoga na anapenda wanaume kauli iliyomshtua Zaidi Kanyari.

Kwa kujiamini, Chokuu alitoa ungamo lake kwa pasta Kanyari kwamba anapenda wanaume na hakuna kinachoweza kubadilisha hilo hata maombi.

Chokuu alizidi kumtoa wasiwasi Kanyari akimwambia kwamba imradi alikubali kupeleka injili yake kwenye TikTok, basi awe tayari kukutana na watu wa kila aina.

“Karibu tiktok pasta. Hii tiktok tulisema tutabanana sote, mapasta, mal**a, watumishi wa Mungu, wote tutabanana hapa hapa. Usiondoke mchungaji. Mimi nimekwambia naitwa chapati pendua,” Chokuu alimwambia Kanyari.

Kanyari alijiunga kweney mtandao wa TikTok yapata mwezi mmoja uliopita na kuwaomba mashabiki wake kumsaidia kuongeza idadi ya wafuasi.

Katika moja ya video yake alipokabiliwa na wana tiktok kuhusu sababu yake ya kuamua kujiunga na mtandao huo ulioharibiwa jina hali ya kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu, Kanyari alijitetea akisema kwamba aliamua kupeleka injili ya wokovu kwa vijana ambao wameshikiliwa na ibilisi TikTok.

Pia mchungaji huyo alikanusha kauli za baadhi ya watu kwamba alifuata pesa TikTok kutokana na zawadi, akisema kwamba nia yake ni kuhubiria na kuponya watu katika ibada zake za mubashara.

Tazama video hiyo hapa Kanyari akitishia kuondoka TikTok;