Pasta Kanyari adai kukosa bahati ya nyota ya mapenzi, “Skendo zangu ni mambo na pesa tu!”

""kendo zangu zote huwa ni mambo ya pesa lakini sijawahi ambiwa mambo ya wanawake sijui kwa nini. Sasa ukisema Kanyari unapenda pesa we unachukia pesa? Tuseme ukweli,” alimaliza .

Muhtasari

• Kanyari alihoji kwa nini kila skendo inayoliandama jina lake ni kuhusu tu mambo na pesa na hajawahi shushiwa skendo kuhusu mapenzi.

MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
MCHUNGAJI VICTOR KANYARI
Image: MAKTABA

Mchungaji mwenye utata, Victor Kanyari ameibuka na madai mapya akidai kukosa bahati katika kupata mapenzi, miaka kadhaa baada ya penzi lake na msanii Betty Bayo kusambaratika.

Kanyari ambaye alikuwa anazungumza kwenye kipindi cha mubashara kwenye tiktok alikuwa anamjibu mmoja ambaye alimwambia kwamba anapenda pesa.

Kanyari alihoji kwa nini kila skendo inayoliandama jina lake ni kuhusu tu mambo na pesa na hajawahi shushiwa skendo kuhusu mapenzi.

Alisema kwamba hata kanisani anapohubiri, hakuna mwanamke hata mmoja amewahi jitokeza na kummezea mate, lakini likija suala la pesa, mara kwa mara jina lake huvutwa kwenye skendo hiyo.

“Sina bahati ya kupendwa na wanawake. Hata katika huduma yangu hakuna wasichana huwa wananicrushia, sijui kwanini. Ndio maana huwa sipati skendo za wanawake. Skendo zangu zote huwa ni mambo ya pesa lakini sijawahi ambiwa mambo ya wanawake sijui kwa nini. Sasa ukisema Kanyari unapenda pesa we unachukia pesa? Tuseme ukweli,” alimaliza akitupa swali kwa aliyemfokea kuwa anapenda pesa.

Nabii huyo mwenye utata alijiunga na TikTok hivi majuzi na amekuwa akifanya vipindi vya moja kwa moja, ambavyo vimekuwa vikimpatia pesa kwa njia ya zawadi.

Baada ya kujiunga kwenye mtandao huwa wa video fupi, Kanyari alikanusha kwamba alifuata pesa kule na kusema kwamba lengo lake kuu ni kupeleka injili kwa vijana, ambao asilimia kubwa ndio wanaotumia mtandao huo.

“Sipo hapa kwa sababu ya pesa. Sipo hapa kwa sababu ninapokea zawadi. Niko hapa kwa sababu napenda TikTok na ninataka kuwaombea wagonjwa na watoto. Kuna watu wanaonewa na shetani, wengine wana matatizo, na wengine wanaishi nje ya nchi lakini hawana furaha. Niko hapa kuwaombea watu hao,” alisema.

Mchungaji huyo katika live ya awali aliwaomba mashabiki wake wa TikTok kumtumia zawadi nyingi, akiomba hadi ile ya Simba ambayo inatajwa kuwa yenye thamani kubwa.