'Wanetu wanajivunia kukuita baba', Diana amsherehekea Bahati kwenye picha ya kifamilia

‘Mpenzi wangu Bahati, mfalme wa The Bahatis, ahsante kwa kuwa baraka katika maisha yetu, wanetu Heaven na Majesty Bahati wanajivunia kukuita baba,’ Diana alichapisha.

Muhtasari

• Mwaka jana, wanandoa hao walisherehekea uhusiano wao kuhitimu miaka 7 huku Bahati akimppa Diana zawadi 7 tofauti kuashiria umuhimu wa wakati ambao ameishi naye.

Familia ya Bahati
Familia ya Bahati
Image: Instagram

YouTuber Diana Marua amemsherehekea mumewe Bahati kwa kupakia picha ya pamoja na wanao huku akimtaja kama baba mwajibikaji kwa wanao.

Diana Marua alichapisha msururu wa picha ya pamoja wakiwa na Bahati na wanao wawili, Heaven Bahati na Majesty Bahati akiiambatanisha na maneno kwamba watoto hao wanajionea fahari kwa Bahati kuwa baba yao.

‘Mpenzi wangu Bahati, mfalme wa The Bahatis, ahsante kwa kuwa baraka katika maisha yetu, wanetu Heaven na Majesty Bahati wanajivunia kukuita baba,’ Diana alichapisha.

Hii si mara ya kwanza kwa rapa huyo kumsherehekea hadharani mpenzi wake na wamekuwa na mazoea ya kuweka maisha yao ya kimapenzi kweney mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, sehemu ya maoni kutoka kwa mashabiki wa familia hiyo walikuwa na haraka kubaini kwamba hakukuwa na picha ya wamano wa kumuasili, Morgan Bahati.

Morgan Bahati, ambaye aghalabu ni mtoto pendwa wa Diana Marua amekuwa akiishi na familia hiyo tangu utotoni na wakati huu ambapo wanafunzi wapo nyumbani kwenye likizo, wengi walihisi kwamba asingekosekana kwenye picha hiyo ya pamoja ya familia.

 

Mwaka jana, wanandoa hao walisherehekea uhusiano wao kuhitimu miaka 7 huku Bahati akimppa Diana zawadi 7 tofauti kuashiria umuhimu wa wakati ambao ameishi naye.