“Mamangu alinifuata na kutaka kuangalia video zangu za uchi zilizovujishwa” - Lukamba (video)

“Mamangu uzuri ni mtu ananisikiliza sana, baada ya kumwambia alisema ‘haya basi’ nikamwambia ‘mama hata wakikuletea usiangalie ni mambo ya kawaida tu si unajua watoto katika hali ya utafutaji maisha.”

Muhtasari

• Akizungumza kwenye mahojiano na Bongo FM, Lukamba alisema kwamba athari ya video hizo za uchi wake ilifikia hatua mbaya kiasi kwamba hata mamake mzazi alizipata taarifa hizo.

Lukamba
Lukamba
Image: screengrab//bongo-fm

Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anajiongeza kama msanii wa Bongo Fleva, Lukamba amefunguka jinsi video zake chafu zilizodaiwa kuvujishwa mitandaoni zilimuathiri si tu yeye bali hadi familia yake.

Akizungumza kwenye mahojiano na Bongo FM, Lukamba alisema kwamba athari ya video hizo za uchi wake ilifikia hatua mbaya kiasi kwamba hata mamake mzazi alizipata taarifa hizo.

Lukamba alisimulia jinsi mamake alimfuata akimuuliza kuhusu video hizo na mbaya Zaidi akasisitiza kwamba anataka kuona lakini mtoto wa kiume anamkatalia mamake asione akisema ni moja ya njia za vijana kutafuta unga.

“Kiukweli imeniathiri kwa namna moja au nyingine kwa Bi mkubwa [mamangu]. Alinipigia simu akiniambia kuwa ameambiwa kuna klipu Mange Kimambo amevujisha, nikamwambia mama acha kuangalia hiyo klipu. Hiyo klipu walinivizia, nikamwambia achana nazo kabisa,” Lukamba alisema.

Msanii huyo hata hivyo alisema kuwa mamake ni mmoja kati ya watu wanamsikiliza sana na hivyo baada ya kumtaka asiangalie, mamake alitii.

“Mamangu uzuri ni mtu ananisikiliza sana, baada ya kumwambia alisema ‘haya basi’ nikamwambia ‘mama hata wakikuletea usiangalie ni mambo ya kawaida tu si unajua watoto katika hali ya utafutaji maisha.”

Video hiyo ilidaiwa kuvujishwa na Mange Kimambi ilitoka kwa mpenzi wake wa zamani na Lukamba alitaja tukio hilo kama silaha iliyokusudiwa kumbomoa kimaadili katika jamii.

“Hapa na pale mtu anaweza akaitumia kama silaha akijua kwamba anaweza akakubomoa, lakini mimi niliwaambia familia yangu jinsi makosa hayo yalivyokuwa na walinielewa na ndicho kitu ambacho namshukuru Mungu kwa kuwa hicho kitu kilikuwa kinanisumbua sana, haswa kwa familia,” Lukamba alisema.