Kingi Tizian afichua kununulia gari lake jipya la Ksh 7M na mwanamke mzungu mweusi (video)

"Mara ya kwanza niliona kama ni mlaghai kwa sababu hajawahi mpa zawadi mtu yeyote TikTok. Kwa hiyo nikasema acha nimpandishe kwenye Live, ni mwanamke mzungu mweusi, alikuja hapo akazungumza kizungu ajabu,” Tizian alieleza.

Muhtasari

•  Hata hivyo kuhusu chanzo cha pesa hizo, Tizian alikanusha kuwa sio pesa za zawadi za tiktok bali ni pesa ambazo alirudishiwa na kampuni ya bima baada ya gari la kwanza kupata ajali.

TikToker King Tizian
TikToker King Tizian
Image: TIKTOK

Wiki moja baada ya kugonga vichwa vya habari baada ya kununua gari jipya, tiktoker King Tizian Savage amefichua gharama ya gari hilo na chanzo cha pesa hizo alizolinunua.

Akizungumza na Oga Obinna, King Tizian alifichua kwamba gari lake ni aina ya Audi A7 ambalo gharama yake ya kulinunua kutoka nje ya Kenya ni shilingi milioni 7.

“Audi ndilo gari la ndoto zangu. Hilo ndio gari likipita ninaliangalia na kulitamani. Langu ni Audi A7. Sasa hivi ukilinunua kutoka nje ya Kenya linakuja na shilingi miioni 7. Bei ya chini kabisa unaweza pata pengine ni 6.5m hivi,” Tizian alisema.

 Hata hivyo kuhusu chanzo cha pesa hizo, Tizian alikanusha kuwa sio pesa za zawadi za tiktok bali ni pesa ambazo alirudishiwa na kampuni ya bima baada ya gari la kwanza kupata ajali.

Alisema kuwa pesa hizo za kampuni ya bima hata hivyo hazingetosha kununua Audi A7 na kufichua kuwa kuliuwa na mkono wa mtu ambaye hamjui ambaye aliingia kwenye kipindi chake cha mubashara na kumuahidi msaada wa pesa za nyongeza ili kununua gari hilo la ndoto zake.

“Kitu ambacho watu hawajui ni kwamba hili si gari langu la kwanza. Unakumbuka kulikuwa na tukio mimi, Prince Mwiti na Chira tulihusika katika ajali ya barabarani mapema Januari? Hilo ndilo gari langu la kwanza na baada ya kupata ajali, nilienda likachukuliwa na nikafidiwa. Lilikuwa ni Audi A6.”

“Halafu pia kuna watu huja kwenye Live yangu, kulikuja tu na mtu kutoka kusikojulikana, mimi simjui, akaniambia kwamba anataka kunipa sapoti ya kupata gari, mara ya kwanza niliona kama ni mlaghai kwa sababu hajawahi mpa zawadi mtu yeyote TikTok. Kwa hiyo nikasema acha nimpandishe kwenye Live, ni mwanamke mzungu mweusi, alikuja hapo akazungumza kizungu ajabu,” Tizian alieleza.

Alisema kuwa mwanamke huyo mara ya kwanza alikuwa anataka kumsaidia kulikarabati gari la Audi A6 lakini baada ya Tizian kumuambia kuwa liliharibika kupita kiasi, aliahidi kumpa pesa za kuongeza ili ununua Audi A7.

“Akaniambia nitumie PayPal yako nione nitafanya nini, mwanzoni yeye alisema alitaka kunisaidia kukarabati gari langu nikamwambia haingewezekana na zile pesa ningepewa nilitaka kununua gari jipya. Kwa hiyo akaniambia kwamba ataniongezea kwa hizo ili ninunue gari jipya. Kwa hiyo aliniongezea,” Tizian alimaliza.