“Sikumbuki mara ya mwisho nilivaa boxer” - Crossdresser Kelvin Kinuthia akiri

Alisema kwamba swali kuhusu yeye kuvaa mavazi ya kiume kulingana na jinsia yake, likiwemo lile vazi dogo la ndani ndilo lilikuwa swali ambalo liliulizwa Zaidi.

Muhtasari

• TikToker huyo aliyejizolea umaarufu mapema 2022 amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa sababu tofauti tofauti.

Kelvin Kinuthia
CROSSDRESSER// Kelvin Kinuthia
Image: instagram

TikToker Kelvin Kinuthia ambaye ni maarufu kwa uvaaji wake wa mavazi kinyume na jinsi yake ameungama kwamba hakumbuki mara ya mwisho alivaa chupi ya wanaume.

Kinuthia alifunguka ukweli wake wakati alikuwa anayajibu baadhi ya maswali kutoka kwa mashabiki wake.

Alisema kwamba swali kuhusu yeye kuvaa mavazi ya kiume kulingana na jinsia yake, likiwemo lile vazi dogo la ndani ndilo lilikuwa swali ambalo liliulizwa Zaidi.

Ili kutupa mwanga katika hilo, Kinuthia alisema kwamba yeye hakumbuki mara ya mwisho alivaa nguo ya ndani ya wanaume.

“Sasa nitajibu aje hili, ukweli ni kwamba sikumbuki mara ya mwisho nilivaa boxer,” Kinuthia alisema.

TikToker huyo aliyejizolea umaarufu mapema 2022 amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa sababu tofauti tofauti.

Licha ya kuwa wa jinsia ya kiume, ni adimu sana kumpata au kumuona Kinuthia akiwa amevalia vazi la jinsia yake, kwani mara nyingi yeye huonekana katika mavazi ya kike na kujipodoa kama mtoto wa kike.

Hivi majuzi, hulka yake ya kuvaa mavazi ya kike licha ya kuwa mwanamume ilizua ghadhabu kwa mchungaji Robert Burale ambaye alimshtumu kwa uvaaji huo na kumtaka kujirudi na kujitambua kuwa yeye ni mwanamume anayestahili kuvaa mavazi ya kiume.

Japo Kinuthia hakumjibu Burale, rafiki yake Mtumba Man alimwakilisha kwa kutoa jibu lake kwa Burale akisema kwamba kuvaa hivyo haifai kuhusishwa na kasumba hasi kwani ni njia tu ya kutafuta riziki na hakuna lingine Zaidi.