Desagu anaeleza kwa nini aliamua kuchukua mapumziko kutoka kwa uundaji wa maudhui

Ukishafanya kitu kwa muda wa miaka 6 au muda mrefu, unakaa chini unajiita mkutano uone kama, mikakati mliyoitumia kama inafanya kazi

Muhtasari

•Ukiwa juu kwanza unarelax hata. Hiyo ni, baada ya miaka 6, wakati mwingine unapumzika, unaenda unapanga mawazo yako upya, na pia umeona tasnia inabadilika.

•Pia kuna projects zingine nafanya kama msanii kuna vitu vingine ambazo nafanya,kwa mfano kuna NGO nafanya kazi nao, pia nafanyanga Digital marketing na consultancy.

Mchekeshaji Henry DeSagu
Mchekeshaji Henry DeSagu
Image: Facebook

 Henry Desagu amefunguka kuhusu ni kwa nini aliamua kuachana na uundaji wa maudhui, haswa kwenye mitandao ya kijamii.

Desagu alisema kuwa uamuzi huo ulitokana na kuwa alijiona kuwa mtayarishaji bora wa maudhui, kwa hivyo alifikiria kuchukua mapumziko, na kujaribu kutengeneza njia zingine mpya za kuunda maudhui.

“Ukiwa juu kwanza unapumzika hata. Hiyo ni, baada ya miaka 6, wakati mwingine unapumzika, unaenda unapanga mawazo yako upya, na pia umeona tasnia inabadilika. TikTok imetokea kila mtu anafanya maudhui si pia wewe lazima ujirebrand upya,” Desagu alieleza.

Alisisitiza umuhimu wa kujitunza na jinsi kuchukua mapumziko haya ni hatua ya lazima kwake na kuongeza nguvu suala zima la kuunda maudhui na kutengeneza pesa,

“Ukishafanya kitu kwa muda wa miaka 6 au muda mrefu, unakaa chini unajiita mkutano uone kama, mikakati mliyoitumia kama inafanya kazi, na ufanye nini tena maana mwisho wa siku dhumuni zima la kutengeneza maudhui ni kupata pesa" Desagu alieleza.

Licha ya kuachana na uundaji wa maudhui ya mara kwa mara, Desagu aliwahakikishia mashabiki wake kwamba huo sio mwisho wake. Amekuwa akifanya kazi zingine ambazo pia zinahitaji umakini wake ndiyo maana amekuwa afanyi kazi ambazo watu walimzoea nazo.

“Pia kuna projects zingine nafanya kama msanii kuna vitu vingine ambazo nafanya,kwa mfano kuna NGO nafanya kazi nao, pia nafanyanga Digital marketing na consultancy. Siwezi kuwa nikifanya kitu kile kile ambacho nimekuwa nikifanya, ninahitaji pia kufikiria mambo ambayo yanajiri.” Desagu alieleza.