Karen Nyamu azungumzia mswada wa fedha, awakashifu Wakenya kwa Kulalamika

"Unazusha nini na ni kitu hata haikuhusu? Tafuta hii Finance Bill inasema nini, kuna tax imeongezwa, inakuhusu?”

Muhtasari

•Karen Nyamu amezua gumzo kwa sababu ya matamshi yake yasiyoeleweka kuhusu Mswada wa Sheria ya Fedha 2024.

•Katika mahojiano, Nyamu alikosoa wale amabo  wanapinga mswada huo, akisema unawalenga matajiri.

KAREN NYAMU
KAREN NYAMU
Image: HISANI

Jaribio la Seneta Mteule Karen Nyamu kueleza yaliyomo katika Mswada wa Fedha wa 2024 liliwaacha wengi wakiwa wamechanganyikiwa huku akijaribu kueleza maoni yake kuhusu Mswada huo.

Katika mahojiano ya video ambayo yamekuwa yakienea yanaonyesha Nyamu akihojiwa kuhusu maoni yake kuhusu Mswada wa Fedha wa 2024. Alifafanua kuwa mswada huo kwa sasa unajadiliwa katika Bunge la Kitaifa, wala si Seneti. Aliwakosoa watu wasio na uwezo zaidi kwa malalamiko yao kuhusu mswada huo, akisisitiza kuwa vifungu vyake vimeundwa kuathiri matajiri, sio wao.

Majibu ya Seneta Nyamu yalikuwa ya wazi bila kutarajiwa kwa mtu wa wadhifa wake.

 "Maoni yangu ya jumla kuhusu Mswada wa Fedha. Kwanza, Mswada wa Fedha unasikilizwa na Bunge la Kitaifa na sio Seneti. Ninachojua kuhusu utawala wa Kenya Kwanza, tulichowaahidi wananchi wa chini ni bottom-up.

Nyamu aliendelea kuelezea maoni yake kuhusu manufaa ya muswada huo, akisema kuwa serikali ilikuwa inatoza ushuru kwa Wakenya matajiri huku ikiondoa mwananchi wa kawaida.

Unaweza kuwa unalalamika kwamba Rais Ruto anatutoza ushuru sana, wakati huo huo Bunge la Kitaifa limeondoa ushuru kwa watu wa kawaida na kuongeza kwa wale wanaoagiza bidhaa kama vitanda kutoka nje ya nchi. "Unazusha nini na ni kitu hata haikuhusu? Tafuta hii Finance Bill inasema nini, kuna tax imeongezwa, inakuhusu?” aliongezea.

Zaidi ya hayo, Nyamu aliendelea kudokeza kuwa mabishano ya mswada huo yalikuwa ni ubunifu wa upinzani na hayana msingi wa ukweli .

“Wachana na mitandao, tuna upinzani na lazima wapige serikali ikuwe wana make sense, wanapiga propaganda, lazima wapige serikali. Na sisi tunawaskiza," alisema.