Manzi wa Kibera aeleza mwanzo mpya wa maisha yake

Ni mimi mpya kabisa. Manzi wa Kibera alikuwa mtu mwingine nilifika mahali sikuipenda."

Muhtasari

•"Umaarufu na pesa hazipelekani sasa hivi najaribu kusafisha brand yangu, socialite siezi kosa kukuwa,  ninajaribu kuwa mshirika mkubwa na chapa safi,”alisema.

•Wambo anadokeza juhudi za siku zijazo kama vile upangaji wa hafla, akipendekeza mwelekeo wa kitaalamu zaidi wa uwepo wake mtandaoni

Dem wa Kibera
Image: Instagram

Manzi wa Kibera, anayejulikana kwa utu wake mitandaoni, ametangaza mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa kutumia mitandao ya kijamii.

Manzi wa Kibera, ambaye jina lake halisi ni Wambo, hivi majuzi alikamilisha kipindi cha maombolezo ya mwanamume ambaye awali alimtambulisha kama mumewe, Mzee Nzioki.

 Tangu wakati huo amekiri uhusiano huo ulifanyika.

Akiashiria sura hii mpya, Wambo amenyoa nywele zake na kuanza kutumia akaunti mpya za mitandao ya kijamii.

 Akiwa kwenye kipindi cha Mungai Eve, alitangaza kuanza maisha mengine kando nay ale ambayo watu wanajua kumhusu.

“Ni mimi mpya kabisa. Manzi wa Kibera alikuwa mtu mwingine nilifika mahali sikuipenda” .

Wambo anasisitiza hamu ya kusonga mbele zaidi ya vitendo vya zamani vinavyotambulika.

 Anaamini mwonekano wake mpya utavutia mikataba ya maana katika Maisha yake.

 akisema, “nilikuwa na jokes mob”

Wambo pia alithibitisha uvumi wa kuwa na mtoto, akielezea nia ya kuzifichua kwa wakati ufaao.

Akikumbuka miaka yake mitano katika kuangaziwa katika mitandao ya kijamii, Wambo anakiri kukosa fursa za ukuaji.

 "Umaarufu na pesa hazipelekani sasa hivi najaribu kusafisha brand yangu, socialite siezi kosa kukuwa,  ninajaribu kuwa mshirika mkubwa na chapa safi,”alisema.

Wambo anadokeza juhudi za siku zijazo kama vile upangaji wa hafla, akipendekeza mwelekeo wa kitaalamu zaidi wa uwepo wake mtandaoni.