Mchungaji Ng’ang’a awatoza waumini ksh 1000 kwa chupa ya maji

Nataka kuona. Nimekupa maji. Na utalipia, kila mtu, kwa KSh 1000. Kila mtu ana deni langu.

Muhtasari

•Kasisi James Ng'ang'a aliamua kuwatoza waumini wake KSh 1000 kwa maji aliyowapa kanisani.

•Mtu wa Mungu alionekana akikusanya haki zake kanisani huku akiwakashifu wale ambao hawakuwa na pesa wakae nyuma.

•Wanamtandao wengi walimkashifu mhubiri huyo kwa 'kuwaibia' maskini, huku wengine wakishangaa jinsi kanisa lake linavyomiminika licha ya tabia yake mbaya.

Nganga
Image: HISANI

Mhubiri James Ng'ang'a alizua gumzo mtandaoni  baada ya kunaswa kwenye video akikusanya noti za KSh 1000 kutoka kwa waumini wake kwa chupa za maji.

Katika video hiyo anahubiri kabla ya kuacha na kuwaambia waumini wa kanisa lake kwamba watalipa KSh 1000 kwa chupa za maji wanazochukuwa.

Alionekana kuwakejeli wale ambao hawakuwa na uwezo wa kutoa pesa hizo huku akiwaambia watoe viatu na pia watakua wanakati nyuma kanisani.

"Nataka kuona. Nimekupa maji. Na utalipia, kila mtu, kwa KSh 1000. Kila mtu ana deni langu. Lete KSh 1000. Lete pesa zangu. Umenighadhibisha. Huwezi kunywa maji yangu bure.

 Kama huna, lete viatu vyako kama huna usikae kwenye safu ya mbele, keti nyuma.” Alisema.

Video hiyo iliwaacha wanamtandao wengi wakilaani mhubiri huyo kwa kuchukua pesa kutoka kwa watu huku akiwaaibisha wale ambao kwa kweli hawakuwa na pesa taslimu za kumpa.

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii:

@harrietkemunto1 said:

 "Strong-arm robbery."

@yungdollar7 said:

 "Kama hauna ukae huko kwa mia mbili."

 @opuravictor said:

 "But walitoa right?"

 @doreen_havilah said:

"Mbona mnakasirisha commander."

@otieno_isss said:

 "I wonder how this church hujaa na congregants."

@unbothered_wairimu said:

"Taxes zikiongezwa we are silent, Ng'ang'a is collecting zake creatively. Robbery without violence. We are so touched by Nganga but not by the Government, mbona mnaumwa?"