Oga Obinna ajizawadia gari mpya aina ya Range Rover kwenye siku yake ya kuzaliwa

Obinna alidokeza kwamba kununua Range Rover ni moja kati ya malengo mengi aliyojiwekea nadhiri kuyatimiza mwaka huu, akidokeza kwamba tayari ametimiza malengo 3 ndani ya nusu mwaka.

Muhtasari

• Hata hivyo, inafaa ikumbukwe kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Obinna kujinunulia gari la kifahari.

Mchekeshaji aliyegeuia ukuzaji maudhui kwenye jukwaa la YouTube, Oga Obinna amejituza kwa njia ya kipekee wakati anaposherehekea kuadhimisha umri wa miaka 34.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obinna alichapisha msururu wa picha akiwa mbele ya gari jipya aina ya Range Rover na kudokeza kwamba ni zawadi maalum aliyojinunulia kwa ajili ya kujisherehekea.

Obinna alidokeza kwamba kununua Range Rover ni moja kati ya malengo mengi aliyojiwekea nadhiri kuyatimiza mwaka huu, akidokeza kwamba tayari ametimiza malengo 3 ndani ya nusu mwaka.

“34 kwenye 4x4 😎🔥. Heri ya Siku ya Kuzaliwa KWA MIMI!! Ni Nusu mwaka na nimetimiza malengo yangu makuu 3 mwaka huu. Ni kweli Mungu ana wakati wake na njia yake ya kufanya mambo.”

Hata hivyo, inafaa ikumbukwe kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Obinna kujinunulia gari la kifahari.

Mnamo 2022, Obinna alijinunulia gari la kifahari aina ya Mercedes Benz na kuonesha furaha yake mitandaoni.

Alitaja Mercedes Benz kuwa ni ishara ya kujithamini kwa kazi ngumu ambayo amekuwa akifanya. 

 

Oga Obinna anajipa zawadi ya gari lingine la gharama kubwa, anaelezea kwa nini

 

“My main chilling with my side😂 haters wanaweza kukufanya ufikiri unapoteza kumbe unashinda usiwaruhusu.

 

"Nimepata ishara hii ndogo ya kujithamini kwa sababu chache," alisema.

 

Aliendelea kuangazia hafla zote muhimu katika maisha yake ambazo zawadi ya gari itawakilishwa.

 

"Kama zawadi Yangu ya Siku ya Kuzaliwa, Kwa Kugonga Wanaofuatilia 100k kwenye YouTube, Kwa Kuwa Hai, Kwa Kuwa Mchapakazi, Kama zawadi ya Krismasi, kama zawadi yangu ya mwaka mpya na hatimaye kuwa katika hali nzuri ya amani ya akili.

 

"Tupande.💥💥 Moja ni ya Kuchafua rada na hii injini ya kusafisha😂. . @magariaffordable 💯👌🏿 Asante kwa kuniletea mtoto huyu  ❤️," Obinna alitaja.