King Kaka aimba wimbo wa Pasta Ng’ang’a akiwaunga mkono Gen Z kwa maandamano

“Wanapanga kutumaliza Baba, kumbe millennials na Gen Z ndio dawa ya washenzi, while mko kwa ma prado zenu ha hizi ma Benz...Lakini surely, renovation Ksh 800m? lakini surely eti tax kwa ma pads?" King Kaka aliimba.

Muhtasari

• Msanii huyo katika wimbo wake alizidi kuwarai vijana kufurika katika mitaa bila mawe.

King Kaka ameendelea kuonyesha mshikamano na Gen Z wanapojitokeza kushiriki maandamano kupinga muswada tata wa fedha 2024.

Msanii huyo amekwenda hatua Zaidi kwa kufanya wimbo wa kiharakati, akitumia wimbo maarufu wa mchungaji James Ng’ang’a “Wanapanga kutumaliza Baba...” akiikosoa serikali kwa baadhi ya vipengele vilivyomo kwenye muswada huo.

Katika wimbo huo ambao ameufanya upya na kuchapisha katika YouTube yake, King Kaka anaanza na kiitikio cha Pasta Ng’ang’a akisema kwamba serikali ina njama ya kuwamaliza wananchi kwa tozo nyingi ambazo zimependekezwa kwa mswada huo.

“Wanapanga kutumaliza Baba, kumbe millennials na Gen Z ndio dawa ya washenzi, while mko kwa ma prado zenu ha hizi ma Benz, Mr President, we haven’t been best friends, ni vile natetea Wakenya wako kwa fence…”

“Lakini surely, renovation Ksh 800m? lakini surely eti tax kwa ma pads? Lakini surely mnatudanganya eti mambo itakuwa shuari? Lakini surely? Hatutaki mu edit, tunasema reject,” King Kaka anaimba kwa sehemu.

Msanii huyo katika wimbo wake alizidi kuwarai vijana kufurika katika mitaa bila mawe.

Muswada wa fedha 2024 umekuwa ukipokea upinzani mkali si tu kutoka kwa wabunge na viongozi wa upinzani bali pia idadi kubwa ya Wakenya wa kila tabaka kwa kile wanahisi vipengele vingi ni vya kupunja mifuko yao.

Muswada huo unatarajiwa kufikishwa bungeni baadae Jumanne kwa marekebisho kabla ya kusukumwa mbele Zaidi na kuwa sheria utakapotiwa saini na rais kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa kifedha mwezi Julai.