Mulamwah, Ruth K wasambaza chai na maandazi bila malipo kwa waandamanaji wa Gen Z Nairobi

Tayari, watu maarufu mbalimbali wameweka wazi msimamo wako kuhusu muswada huo tata, wengi wao wakionekana kusimama na vijana walio wengi kupinga muswada huo.

Muhtasari

• “MANDUNYA ZIKO READY , energy kwa wingi . tupatane CBD . usipofika unatuangusha sana . lets fight as a unit . #RejectFinanceBill2024” Mulamwah aliandika kwenye chapisho hilo.

Huku maandamano ya vijana wa Gen Z yanapozidi kushika kasi katika mitaa mbali mbai, mchekeshaji Mulamwah na mpenzi wake Ruth K wamejitokeza kushiriki maandamano kwa njia nyingine tofauti.

Mulamwah na Ruth K walipakia picha wakiwa na ddoo kadhaa zilizojaa maandazi pamoja na chai na kusema kwamba ni kwa ajili ya waandamanaji ambao wamekuwa wakimenyana na polisi katika mchezo wa paka na panya katikati mwa jiji la Nairobi.

Mulamwah alitumia fursa hiyo kuwarai vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki maandamano hayo yanayonuia kupinga kupitishwa kwa mswada wa fedha 2024, akisema kwamba ambaye hatojitokeza atakuwa anawakosea vijana wenza wanaoandamana.

“MANDUNYA ZIKO READY , energy kwa wingi . tupatane CBD . usipofika unatuangusha sana . lets fight as a unit . #RejectFinanceBill2024” Mulamwah aliandika kwenye chapisho hilo.

Maandamano ya wakati huu yamekuwa tofauti kidogo kwani hayajaongozwa na mwanasiasa yeyote bali ni vijana waliojikusanya wenyewe bila kiongozi katika mitandao ya kijamii na kuitana kwa wingi kushiriki maandamano hayo.

Tayari, watu maarufu mbalimbali wameweka wazi msimamo wako kuhusu muswada huo tata, wengi wao wakionekana kusimama na vijana walio wengi kupinga muswada huo.

Muswada huo unatarajiwa kufikishwa katika bunge la kitaifa baadae leo kwa kusomwa mara ya tatu baada ya kundolewa kwa baadhi ya vipengele vilivyopata pingamizi nyingi.

Hata hivyo, vijana hao waandamanaji wanataka muswada huo kutupiliwa mbali kabisa walac si kunyofolewa kwa baadhi ya vipengele.