Daddy Owen afunguka kwa nini anataka kuoa msichana wa kijijini

Owen alisema mama yake anamshinikiza atafute mtu wa kumtembelea naye.

Muhtasari

•Akizungumza na Word Is, Owen alisema ana shinikizo kwamba umri wake unasonga na bado hana familia yake.

•"Nataka mtu ambaye atakuwa wangu na si wa dunia nzima. Nataka mtu ambaye atazingatia kabisa ndoa yetu, na kunitengenezea milo ya kitamaduni." alisema.

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen ana wasiwasi kuhusu kutopata watoto wengine.

Akizungumza na Word Is, Owen alisema ana shinikizo kwamba umri wake unasonga na bado hana familia yake.

Owen alisema mama yake anamshinikiza atafute mtu wa kumtembelea naye.

“Ananiambia hata niajiri mtu ili tu niache kutembea peke yangu nyumbani,” alisema.

"Ana wasiwasi kwamba ninaishi peke yangu, natembea peke yangu."

Owen, 40, alisema kwa sasa alitazamia kuwa amemaliza kupata watoto.

"Sijajiandaa kwani naelewa sio uamuzi wangu peke yangu, nahitaji kuwa na mtu." Owen alisema kuwa hata akiwa na pesa, hajakamilika.

Alipoulizwa kama anachumbiana, Owen alisema bado anahofia kwamba huenda asifanye vyema baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika.

"Hatua yoyote na mtu mwingine kunaweza kuleta kumbukumbu za maisha yangu ya nyuma. Najiuliza kama, nitamtendea vizuri au nitakuwa chini ya shinikizo sawa na mahusiano yakaisha tena?"

Alisema anataka kuchumbiana na msichana wa kijiji wakati huu.

"Natafuta mwanamke makini wa kuchumbiana naye na kuoa, natafuta mwanamke mwenye ngozi nyeusi, muombaji sana, awe wa kijijini," alisema.

Alisema hiyo ndiyo sababu anatembelea mara kwa mara na kuendesha miradi vijijini.

"Nataka kupata mwanamke kutoka huko. Sitaki kuchumbiana na mtu ambaye amezaliwa mjini," alisema.

Pia hataki kuchumbiana na mtu mashuhuri.

"Sitaki mtu ambaye kila mara yuko kwenye mitandao ya kijamii. Staki mtu wa TikTok," alisema.

"Nataka mtu ambaye atakuwa wangu na si wa dunia nzima. Nataka mtu ambaye atazingatia kabisa ndoa yetu, na kunitengenezea milo ya kitamaduni."

Kuhusu jinsi anavyovaa, Owen alisema mwanamke wake hatavaa suruali ndefu.

"Nataka mtu anayevaa nguo ndefu," alisema.

Kwa sasa Owen anashughulika na kuzindua nyumba ya watoto huko Eldoret ifikapo Desemba.

"Watoto wenye ulemavu walinipa msukumo wa kufanya mradi huo, na nataka mahali pa kudumu waweze kufuatiliwa vyema katika safari yao ya afya," alisema na kuongeza kuwa elimu ya watoto hao itatolewa huko.

Ufadhili wa mradi huo ulifanywa na Wakfu wa Safaricom na kugharimu takriban Sh30milioni.

Kimuziki, Owen anafanya kazi na wasanii wadogo kwa vile anataka kuibua vipaji vyao na kuwashauri.

"Nataka kupata vibe ambayo iko kwenye tasnia ninapowashauri ili kupata uzoefu," alisema.

Utafsiri: Samuel Maina