Harmonize amvizia malkia wa Jamaica, Spice kwenye chumba cha hoteli akiwa nusu uchi

"Siamini. Jamani, niamsheni. Je, ninaota?.. Asante sana" Harmonize alisema baada ya kukutana na Spice.

Muhtasari

•Harmonize amedokeza anafanya wimbo na malkia wa dancehall wa Jamaica Grace Latoya Hamilton almaarufu Harmonize.

•Harmonize alimshukuru malkia huyo wa dancehall na kudokeza kwamba amekuwa akisubiri kwa muda mrefu kukutana naye.

Harmonize na Spice wakirekodi video
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo, Harmonize amedokeza kwamba anafanya wimbo na malkia wa dancehall wa Jamaica Grace Latoya Hamilton almaarufu Harmonize.

Siku ya Jumatano, wawili hao walikutana jijini Miami, Marekani ambapo walikuwa na kipindi cha kurekodi video ya wimbo. Konde Boy alishiriki baadhi ya matukio ya kipindi hicho kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kabla ya kuelekea kurekodi video katika kidimbwi cha kuogelea, wanamuziki hao walionekana kufurahi sana kukutana kwa mara ya kwanza. Katika video aliyochapishwa na Harmonize, staa huyo wa bongo fleva alionekana akielekea kwenye mlango wa chumba cha hoteli cha Spice huku akiwa amevalia kaptula fupi tu na wote walionekana kufurahi sana na kukumbatiana baada ya kukutana.

"Hatimaye, habari yako? Wangwan," Spice alimwambia bosi huyo wa Konde Music Worldwide baada ya kumfungulia mlango.

Harmonize ajawa bashasha kukutana na Spice
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Harmonize alimshukuru malkia huyo wa dancehall na kudokeza kwamba amekuwa akisubiri kwa muda mrefu kukutana naye.

"Siamini. Jamani, niamsheni. Je, ninaota?.. Asante sana (Spice). Hii ina maana kubwa kwangu. Tumefurahi sana na hii ina maana kubwa kwangu," Harmonize alisema.

Mwimbaji huyo wa Tanzania alisema kuwa kufanya wimbo na Spice ina maana kubwa, si kwake tu bali kwa bara zima la Afrika.

Harmonize amekuwa Marekani siku kadhaa zilizopita ambapo amekuwa na vipindi kadhaa na vipindi vya kurekodi muziki. Anaonekana kuwa pamoja na anayedaiwa kuwa mpenzi wake mpya Phiona almaarufu Yolo the Queen.

Mapema mwezi huu, staa huyo wa bongo alitangaza wazi kwamba hayupo single tena baada ya kusubiri ,miezi kadhaa.

Takriban miezi mitano baada ya kutengana na muigizaji wa filamu bongo Frida Kajala Masanja, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimtambulisha mwanasosholaiti wa Rwanza Phiona kama mpenzi wake mpya.

"Sawa, siko single tena nimechukuliwa tayari," mwimbaji huyo alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Konde Boy alidokeza amemfahamu Phiona kwa miaka minne iliyopita akitaja kuwa ni wakati mwafaka wa kujaribu mahusiano.

Huku akionekana kuwatupia vijembe wapenzi wake wa zamani k.m Kajala Masanja, Wolper na Sarah Michelloti, alibainisha kuwa mwanasosholaiti huyo wa Rwanda ni zaidi ya wanawake wote ambao aliwahi kuchumbiana nao.

"Naona ni wakati wa kukuonyesha jinsi nilivyo mwanaume wa kweli. Nakupenda sana Yolo The Queen. Umepita kila msichana niliyekutana naye maishani mwangu. Umenifanya hata nijisikie kuwa mimi ni Mnyarwanda," alisema.

Aliendelea kudokeza kwamba hata anapanga kununua nyumba nchini Rwanda ili mradi tu kuwa karibu na mpenzi wake mpya.

Ili kuthibisha mapenzi yake kwa mlimbwende huyo, staa huyo wa bongo fleva alidokeza kwamba anapanga kuchorwa tattoo yake ambayo kulingana naye, itakuwa ya mwisho kabisa kuchorwa mwili mwake.

"Sawa, napata tattoo yangu ya mwisho. Sitokuja choraga tena. Bila shaka ni ya uso wako mzuri Phiona," alisema.