Lilian Nganga hatimaye afichua jina la mwanawe na Juliani

Utheri ni jina la Kikuyu linalomaanisha 'Mwangaza.'

Muhtasari

•Mke huyo wa Juliani amesema mtoto huyo wake wa kwanza amemletea furaha kwa kufanya aitwe mama.

•Huku akiadhimisha miezi wa pili wa mwanawe Lilian pia alifichua kuwa jina la mtoto huyo wake ni 'Utheri'


Aliyekuwa mke wqa gavana Mutua
Lilian Ng'ang'a Aliyekuwa mke wqa gavana Mutua
Image: Instagram

Lilan Ng’ang’a amesherehekea miezi miwili baada ya kuzaliwa kwa mwanawe aliyezaliwa Julai tarehe 22.

Mke huyo wa Juliani amesema mtoto huyo wake wa kwanza amemletea furaha kwa kufanya aitwe mama.

“Nimeingoja siku hii kwa hamu na ghamu, singengoja kukuche ili niione tabasamu ya mwanangu anapotimiza miezi miwili,”alisema Lilian.

Huku akiadhimisha miezi wa pili wa mwanawe Lilian pia alifichua kuwa jina la mtoto huyo wake ni 'Utheri'

“Utheri, kijana wangu,”alisema.

Utheri ni jina la Kikuyu linalomaanisha 'Mwangaza.'

Haya yamejiri siku moja tu baada ya mke huyo wa zamani wa mwanasiasa Alfred Mutua kuwajibu wakosoaji ambao wamekuwa wakimkejeli.

"Nimeona hadithi isiyo na kina ambayo kila mtu anajaribu kunivuta. Kweli hamchoki...Endeleni tu. Acha niendelee na siku yangu na mtoto wangu mdogo,” Lilian Ng’ang’a alijibu.

Siku ya Jumatano mume na mzazi mwenza wa Bi Lilian, Julius Owino almaarufu Juliani kuzua gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukiri kwamba anakabiliwa na changamoto za kifedha.

Katika taarifa ya video ambayo alitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Juliani hata hivyo alibainisha kuwa bado hajafilisika.

"Katika miaka mitatu iliyopita nimekuwa nikiweka pesa zangu kwa kila kitu nilichofanya. Sina wafadhili, sina wawekezaji, sina chochote. Nimeweka pesa zangu kidogo kwa ajili ya hayo," alisema katika video aliyopakia Twitter.

Rapa huyo alidokeza kwamba hata alichukua madeni kadhaa katika juhudi za kukamilisha baadhi ya miradi yake.

Aidha alifichua kuwa changamoto za kifedha zinazomkabili kwa sasa zimesababisha yeye kukosa muda wa kuwa mwanawe huku akimshukuru mkewe na mzazi mwenzake Lilian Nganga kwa kumuelewa.

"Siwezi kupata muda na mwanangu sasa kwa sababu nahangaika huku na kule nikijaribu kulipa madeni niliyochukua ili kutimiza mambo kadhaa ambayo nilijiahidi kutimiza. Namshukuru sana mama (Lilian) kwa kuelewa ninachojaribu kufanya," alisema.

Juliani hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto za kifedha bado hajafilisika kwani angali anaweza kukidhi mahitaji muhimu.

"Mkiniona nikihangaika sifanyi, sifanyi hayo yote kwa ajili yangu mwenyewe. Niko sawa , kuna paa juu yangu naweza kujilisha lakini niko na ndoto zangu," alisema.

Baadaye, babake mtoto na mpenzi wake Lilian kuiweka hadharani kuwa wako na ‘shida’ ya kifedha.

Katika chapisho lake la utani Jumatano asubuhi, Juliani alidai kuwa amefilisika na kuwaomba Wakenya kumchangia pesa za kununua nepi  za mwanawe mdogo kupitia Mpesa.

Alijitambulisha kama rapa  na mjasiriamali anayeteseka.